Gari aina ya DCM linalofanya safari zake kati ya Gongo la Mboto na Masaki jijini Dar es Salaam likiwa limeinuliwa baada ya kupinduka leo mchana eneo la Kipawa Njia Panda ya Jet Lumo, Dar es salaam. 
Chanzo cha ajali hiyo kinadaiwa ni kumkwepa mwendesha baiskeli. Watu kadhaa wanadaiwa kufariki dunia na wengine zaidi ya 50 wamelazwa katika hospitali za Amana na Muhimbili.
 (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
 Wananchi wakiliangalia paa la gari hilo lililokatwa kwa kupata urahisi wa kuwatoa majeruhi waliokuwemo kwenye gari hilo

 Lenzi ya jicho la blog ya ujijirahaa ilipata kuona katika ajali hiyo kitu kinacho sadikika ni hirizi iliyokua juu ya Gari hilo imeshonwa kwa nyuzi nyeusi iliyovishwa kitambaa cheusi
Gari hilo likitarajiwa kuvutwa kuondolewa eneo la tukio

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...