Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
UONGOZI wa klabu ya Simba ya Jijini Dar es Salaam umesema kuwa hawawezezi kushushwa daraja kwa ajili ya deni la mchezaji wao wa zamani Donald Musoti ambalo lipo ndani ya uwezo wao.
Musoti amechezea Simba msimu wa 2014/15 na kuachwa amelalamika FIFA kwa kumtumia mwanasheria wake Felix Majani, FIFA ambayo imeona Musoti ana hoja, hivyo Simba imetakiwa kumlipa Sh 64.2 milioni.
Rais wa klabu hiyo Evance Aveva amesema kuwa klabu yao haiwezi kushindwa deni hilo la Musoti kwani wameshaanza kulizungumza kabla ya kupokea barua kutoka FIFA.
"Tulianza vikao takribani siku tatu nyuma kabla ya kupokea barua kutoka FIFA na tumebakiwa na mwezi mzima na tutahakikisha tunalipa deni hilo", amesema Aveva.
Akizungumzia kuhusu fedha za mauzo ya mshambuliaji wao Emmanuel Okwi Aveva amesema kuwa fedha hizo zimeshaingia na zitatumika kwa ajili ya masuala ya ndani ya Simba.
"Simba ni taasisi na suala la fedha za mauzo ya Okwi zitajadiliwa na ndani ya vikao vya mapato na matumizi na tutahakikisha zinatumika kama zilivyopangwa", amesema Aveva.
Amesema yapo masuala mengi ya ndani ya klabu ikiwemo ujenzi wa uwanja wa Bunju ambao ulikuwa unasubiri mvua zimalizike.
"Uwanja wa Bunju ulishindwa kushughulikiwa kwa kipindi kirefu kutokana na kusubiri fedha hizi na zimeshaingia na tumekubaliana kuanza ujenzi mara moja, "amesema Aveva.
Pia ametoa msimamo wa klabu kwa kuwashughulikia wachezaji watano wa kimataifa kwa kosa la kusema uongo na kutokuhudhuria kambini kwa madai ya kutokulipwa mishahara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...