Katibu Mkuu Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Mpoki Ulisubisya ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kuboresha maslahi ya watumishi wake na kuendelea kuweka miundombinu bora ya kiutendaji.Akizindua Baraza la Wafanyakazi la Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dk. Ulisubisya amesema hatua hiyo ni ya kupongezwa kwani inampa motisha mtumishi kufanya kazi kwa bidii.
“Nimefarijika sana kuoana suala la maslahi ya watumishi linapewa kipaumbele hapa MNH kwa kweli mnastahili pongezi na taasisi nyingine hazina budi kuiga mfano huu, lakini napenda kusisitiza kuwa kila mtumishi ni vema akanufaika na maboresho haya amesema,” Dk Ulisubisya.
Akizungumza kabla ya uzinduzi wa baraza hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Lawrence Museru amesema hivi sasa hospitali hiyo imeongeza mapato yake kutoka Shilingi Bilioni 2 hadi kufikia Bilioni 4.
Pia amesema katika kuendelea kuboresha huduma za matibabu MNH ina mpango wa kuongeza ICU ya watoto wadogo pamoja na ICU ya kina mama wenye matatizo ya uzazi ili kuokoa maisha ya mama na mtoto .Kwa mujibu wa Profesa Museru Hospitali hiyo ipo katika hatua za mwisho za kupata mkopo kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkopo ambao utasaidia kupanua huduma za afya ikiwamo kununua vifaa tiba vya upasuaji.
Katika kikao, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wamemchagua Dk. Kissa Mwambene kuwa Katibu wa Baraza hilo pamoja na Eneza Msuya kuwa Katibu Msaidizi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki
Ulisubisya akizungumza na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili (MNH) LEO. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi
Janabi, Katibu wa baraza hilo, Dk Kissa Mwambene. Kushoto ni Mwenyekiti
wa baraza hilo na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru na Mkurugenzi wa Rasilimali
Watu wa MNH, Makwaia Makani.PICHA NA JOHN STEPHEN, HOSPITALI YA TAIFA YA
MUHIMBILI (MNH)
Wajumbe
wa Baraza la Wafanyakazi Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) wakipiga
makofi wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo Jinsia, Watoto
na Wazee, Dk Mpoki Ulisubisya wakizungumza na wajumbe wa baraza hilo Leo
kwenye hospitali hiyo.
Kutoka
kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi wa hospitali hiyo, Dk Kissa
Mwambene, Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Lawrence Museru, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya na Maendeleo, Jinsia, Watoto na Wazee, Dk Mpoki
Ulisubisya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya
Kikwete (JKCI), Profesa Mohamedi Janabi, Katibu Msaidizi wa baraza hilo,
Wakili Eneza Msuya na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa MNH, Makwaia
Makani.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...