Kwa takriban miaka mitatu sasa mtu asiyefahamika na ambaye anasadikiwa ana changamoto ya ufahamu wa akili ,anaishi katika upenyo wa mnara wa saa hiyo iliopo katika makutano ya barabara za Nkrumah, Relwe na Samora katikati ya jiji la Dar es salaam. Hapo anapika, anakula, anafua nguo na analala, ikiwa ni robo kilomita tu kutoka makao makuu ya halmashauri ya jiji. 

Kama hiyo haitoshi mnara huo uko katika hali mbaya na bustani yake inatia huruma. Mnara huu ulijengwa miaka takriban 85 iliyopita kama kumbukumbu ya  Dar es salaam kufanywa jiji.Wahusika mpo?

ANGALIZO: Je, una kijipu upele kinachowasumbua au kukukera huko uliko popote Tanzania? Tutumie na maelezo kamili kwa;
 Whatsapp namba 0754271277 
ama email issamichuzi@gmail.com
TUTAKIRUSHA MARA MOJA! 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. AnonymousMay 17, 2016

    Hapa clock tower ni central business district afadhali waliondoa jengo moja hapo lilikuwa limechakaa sana, hii saa yenyewe haipendezi wakati mwingine nikipita hapo natamani jiji lingenunua saa nzuri za plastic. Kijipu cha hapo chini nacho ofisi ya jiji inayohusika ikishughulikie haraka hizi round about ziboreshwe ni kioo cha mji kwa wageni wanaoingia zikiwa na upungufu haifai.

    ReplyDelete
  2. AnonymousMay 17, 2016

    AIBUU!!

    ReplyDelete
  3. kiukweli hapo mahali mnara wa saa maaruf 'clock tower' hapana mvuto kabisa siku hizi, huyo kijana ni mvuta bangi tu masikini, wakati mwingine kama hajapata anakuwa mpole akishalikoleza anapanda huko juu na kuanza kuimba nyimbo za Bob marley kwa sauti ya juu haswa, hata ukipita chini unakuwa na hofu ya usalama wako kwani aweza kukutupia chochote.

    ReplyDelete
  4. Jipu Kubwa ni ile ya sanamu wa Askari kwenye round about ya Samora Avenue na Maktaba street, Ile ni Sanamu ya kumbukumbu ya Waafrika wenzetu walopigana WWI kumsaidia Mwingereza in British Carrier Corps Soldiers. Sasa maana yake sisi tunafurahia wenzetu(watumwa) waliopigania kumsaidia mwingereza(mkoloni) dhidi ya maadui zake kwenye WWI ni upumbavu mtupu. Yaani wenzetu wamekufa,wameumia kwa kutumikishwa matakwa ya Bwana(mkoloni) halafu sisi tunawekewa sanamu na waingereza kwa kuwa watiifu kwa Bwana. Na kabla ya hiyo sanamu kulikuwa na sanamu ya Governor wa Kijerumani East Africa(Hermann von Wissmann) Mkono mmoja Kajishika Hip na mwingine kashika jambia halafu chini kuna Askari mmbongo anam-cover dead lion Waingereza walipoingia Dar mwaka 1916 wakaivunjilia mbali. Ile sanamu inabidi ivunjwe iwekwe ya Mwalimu Nyerere tena picha iwe siku anapewa Uhuru wakati bendera ya Tanganyika inapandishwa na ya Mkoloni mwingereza inashushwa. Hilo ndo Jipu Langu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...