WIZARA Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeandaa mafunzo kuhusu zana ya mawasiliano ya mawasiliano ya kuzuia ukatili dhidi ya watoto kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii na badhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii 42 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke. Madhumuni ya mafunzo haya ni kujenga uwezo wa maafisa hao ili kuongeza uelewa na mbinu za malezi katika familia.
Wizara imewataka maafisa hao wakawe chachu ya kuhamasisha jamii kuwapatia watoto haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na haki ya kulindwa ili kutokomeza ukatili dhidi ya watoto hapa nchini.
Mtoa maada akifundisha mbele ya Maafisa Maendeleo ya Jamii na badhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii 42 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam semina hiyo inayoendelea kufanyika katika ukumbi wa Taasisi ya elimu ya Dar es Salaam.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na badhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii 42 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakimsikiliza mtoa maada.
Maafisa Maendeleo ya Jamii na badhi ya Maafisa Ustawi wa Jamii 42 kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Temeke wakiwa katika picha ya pamoja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...