Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Issaya Mngurumi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo na kuhusiana na kuwaondoa wafanyabiashara wanaofanya biashara maeneo yasiyo rasmi hasa barabarani, Amesema kuwa wafanyabiashara hao maarufu kama machinga wanatakiwa kuondoka ifikapo Mei 8 mwaka huu na kuwa wametafutiwa maeneo kwa ajili ya shughuli za biashara ndogondogo hasa katika maeneo ya Kigogo Fresh, Soko la Tabata Muslimu na eneo lililopo Mkabala na Gereza kuu la Ukonga, Pia amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo watakaohusika ni wale ambao wametambuliwa na kuorodheshwa kutoka maeneo ya Kariakoo, Karume, Buguruni, Ukonga Mombasa, Jangwani, Kibasila, Banana na Gongolamboto.

Mngurumi amesema kuwa wafanyabiashara ndogondogo 2961 wameshatambuliwa na kuorodheshwa  ili waweze kuhamia kwenye maeneo yaliyoandaliwa kwa ajili yao.

Wafanyabiashara ndogondogo wametakiwa kutekeleza agizo la kuondoka katika maeneo hayo na kwenda maeneo  ambayo watakayogawiwa ifikapo Mei 8 mwaka huu.  Kushoto ni Afisa Mipango miji mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Issaya Mngurumi,kulia, Afisa Mipango miji mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala, Paul Mbembela(Katikati) na Afisa Afya Halmashauri ya Ilala, Charles Wambura wakiwa katika mkututano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...