Na Bashir Yakub.
1.NINI MAANA YA KUUMIA KAZINI.
Kuumia kazini kunajumuisha kila jeraha analolipata mfanyakazi wakati akitekeleza majukumu yake ya kazi. Jeraha laweza kuwa dogo au kubwa lakini litaitwa jeraha tu. Katika maana hii yapo mambo mawili kwanza jeraha na pili wakati ukiwa kazini. Ili mfanyakazi apate stahiki zake ni lazima haya mawili yatokee.
( a ) JERAHA HUJUMUISHA NINI.
Jeraha ni pamoja na kidonda, kukatika kiungo iwe mkono , mguu, kidole au vinginevyo, kuathirika akili, magonjwa yaliyotokana na kazi kwa mfano kansa inayotokana na kemikali za viwanda, magonjwa ya ngozi, na athari nyingine za kimwili au kiakili zilizotokea wakati mfanyakazi akiwa kazini au zilizosababishwa na kazi ya mfanyakazi.
( b ) NI WAKATI UPI NI WA KAZI.
Wakati wa kazi ni wakati wote ambao mfanyakazi atakuwa akitekeleza majukumu yake ya kazi kwa mujibu wa ratiba ya ofisi. Kuumia ukitekeleza kazi za kiofisi nyumbani kwako hakuwezi kuhesabika kama kuumia kazini /wakati wa kazi.
Lakini kuumia ukiwa safarini kuelekea mkoa au nchi fulani kutekeleza majukumu ya kazi ni kuumia wakati wa kazi. Hii ndiyo tafsiri yake.
Hongeara sana kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii yetu.
ReplyDeleteIla pia tunaomba utupe darasa la wanaoumia wakiwa kwenye magari ya binafsi au ya abiria.
Maana nchi za wenzetu ukiumia ndani ya magari ya abiria bima zao zinatoa malipo ya pesa za hospital(matibabu ) na pesa za kujikimu kimaisha wakati unajiuguza kabla ya kurudi kazini. Lakini sijawahi ona Watanzania wanalipwa malipo kama haya kwenye ajali nyingi zinazotokea.
Hii itasababisha wananchi kudai haki zao kupitia bima ya gari pindi ajali zinapotokea.Pia itafanya madereva kuwa makini wakiwa na abiria.