Na  Bashir  Yakub. 

KUTELEKEZA WATOTO/MTOTO. 
Ni  kosa la jinai. Ni kinyume  na kifungu  cha   166 cha Kanuni  za  adhabu.  Adhabu  yake  ni  kifungo  cha  miaka  miwili. Kosa  linamhusu  mzazi, mlezi, au  mwingine  yeyote aliye na jukumu  la  kuangalia  watoto/mtoto.

KUKATAA  KUMPA  CHAKULA   NA NGUO MTOTO. 
Ni  kosa la  jinai. Ni  kutokana na   kifungu  cha  167   cha  kanuni  za  adhabu. Adhabu  yake  ni  kifungo cha miaka  miwili.  

KUMNYIMA CHAKULA NA NGUO  MTUMISHI. 
Ni  kosa la jinai. Ni kutokana na  kifungu cha  168 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo  cha miaka miwili. Watumishi wa hapa  ni  wale  wanaotegemea  matajiri  wao  kama  wale  wa wafanyakai wa ndani n.k. 

UKATILI  KWA  WATOTO. 
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha 169A cha kanuni za adhabu. Adhabu  yake  ni kifungo  kisichopungua miaka mitano na kisichozidi miaka kumi na tano.
KUHARIBU MTOTO. 
Ni kosa la jinai. Ni kutokana na kifungu cha  219( 1 ). Adhabu yake  ni kifungo cha  maisha.

KUFICHA  KUZALIWA KWA MTOTO. 
Ni  kosa  la jinai. Ni kutokana  na kifungu  cha  218 cha kanuni za adhabu. Adhabu yake ni kifungo cha miaka  miwili.

KUJARIBU KUJIUA. 
Ni kosa la jinai. Ni kutokana  na  kifungu  cha 217 cha kanuni  za adhabu. Adhabu yake ni  kifungo cha miaka miwili.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...