Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Emmanuel Humba, (kulia), akimkaribisha Naibu Waziri wa Kazi Mhe. Anthony Mavunde alipowasilili kufungua mafunzo kwa Madaktari yanayohusu ajali na maginjwa yanayosababishwa na kazi Jijini Arusha Leo. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), umeendelea na kampeni yake ya kutoa mafunzo kwa madaktari ili kujenga uelewa wa kufanya tathmini ya ajali na magonjwa ayapatayo mfanyakazi yanayotokana na kazi safari hii ikihusisha madaktari kutoka mikoa mitano ya ambayo ni Arusha Tanga, Manyara, Kilimanjaro na Singida.

Mafunzo hayo yaliyofunguliwa leo Mei 30, 2016 na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, huko jijini Arusha, ni muendelezo wa mafunzo mengine kama hayo yaliyotolewa wiki mbili zilizopita jijini Dar es Salaam, ambapo madaktari kutoka mikoa ya Dares Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, lindi na mtwara walihudhuria. 

WCF imechukua hatua hiyo ili kujiandaa na UTOAJI WA Mafao kwa mara ya kwanza tangu uanzishwe ifikapo Julai mwaka huu wa 2016.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu Wenye Ulemavu, Bw. Anthony Mavunde, akizungumza kwenye Mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...