Msemaji wa TFF , Alfred Lucas.

Na Zainab Nyamka,Globu Ya Jamii.
TIMU ya Taifa ya Misri  inatua chini kesho kwa ajili ya kuvaana na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa stars) katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) huku   waamuzi wa mchezo huo wakitoka nchini Gabon na timu hizo zitashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa kwenye mchezo huo utakaopigwa Juni 4 mwaka huu.

Misri ambao wamezoea kuzifunga timu za ukanda wa Afrika mashariki wanatuanchini wakiwa na jumla ya pointi saba huku Stars wakiwa na pointi moja  na katika kuelekea mchezo huo Stars ndiyo haswa itakayohitaji kuibadilisha karata ya mafarao hao kwani kwa hali yeyote kikosi cha timu hiyo kitakuwa inahitaji kuibuka na ushindi tu, kazi ambayo wachezaji itawabidi waoneshe kiwango chao cha juu ili kuweza kupata mabao mengi.

Endapo  Stars itapata matokeo mazuri katika mchezo  huo na Misri itakuwa imejiweka pazuri kwenda kuikabili Nigeria Septemba mwaka huu na Kocha Mkuu wa  Stars Charles Boniface Mkwasa atakuwa akihitaji ushindi ambapo yupo  katika hali ya matumaini na mbinu atakazotumia kuibika na ushindi katika mchezo huo kwani amesifia maandalizi yanayofanyika kuelekea mchezo huo.

"Timu tayari imetoa sare ya bao 1-1 dhidi ya Harambee Stars katika mchezo uliochezwa katika nyasi za ugenini nchini Kenya hiyo ni hatua nzuri katika kuelekea kuona mapungufu ya timu yangu ,"alisema Mkwasa.

Mchezo wa mataifa yote mawili utakuwa ni mchezo utakao hamua nani ataendelea katika fainali hasa kwa Misri ambayo ikipata sare ya bao moja moja itakuwa imejihakikishia kutinga katika fainali hizo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...