Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha cha Dar es salaam, wameendelea na Mgomo wao hadi muda katika Hostel za Mabibo jijini Dar es salaam, wakiishinikiza bodi ya mikopo kutoa fedha za kujikimu. 

Makamu wa Rais wa serikali ya wanafunzi, Shamila Mshangama amesema mgomo huo ni matokeo ya taarifa zisizoeleweka zilizokuwa zikitolewa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kuhusu lini fedha hizo zitatolewa.

Inadaiwa kuwa pesa hizo kwa kawaida huingiziwa kila baada ya siku 6o, lakini mpaka sasa ni wiki mbili zaidi ya muda ambao pesa hiyo ilitakiwa iwe imeingizwa.


Mgomo huo ulioanza saa mbili asubuhi leo ambapo mpaka sasa haujakoma kutokana na msimamo wa wanafunzi hao wa kutoacha kugoma mpaka watakapopatiwa haki yao.

Akizungumza na waandishi wa habari Prof. Rwekaza Mkandara, Makamu Mkuu wa UDSM alisema kuwa,  fedha hizo zingetolewa kabla ya kufika Saa 12 jioni.

Awali msimamo wa wasomi hao ulikuwa ni kuwataka Viongozi wakuu wa Mkoa wa Dar es salaam, ili kuzungumza nao.

Tutaendelea kujuzana zaidi kadri taarifa zitakavyokuwa zikitufikia.
Wanafunzi wa chuo kikuu Dar es salaam (UDSM), wakiwa katika eneo la Cafeteria maarufu Kama Revolution Square, katika Mabweni yao ya Mabibo jijini Dar es salaam wakiwasikiliza viongozi wao

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. IMERUDI TENA HIYO WAMAOHUSIKA WAWALIPE WANACHUO HAO

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...