Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa

Na Zainab Nyamka, Blogu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema kwamba mchezo ujao kati ya Mapharao wa Misri na Taifa Stars, utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika AFCON hapo mwakani kutoka kundi G.

Akizungumza mara baada ya kuwasili hapa nchini kutoka nchini Kenya, Mkwasa amesema timu yake imeweza kucheza vizuri ingawa kuna makosa madogo madogo yaliyojitokeza lakini yatafanyiwa marekebisho na ukiangalia kikosi cha  Harambee Stars kilikuwa na wachezaji sita wakulipwa na waliweza kucheza nao na wakapata goli mapema lakini wao wakaja kurudisha kwa mkwaju wa penati.

 “Najua Misri wanatufuatilia na hata Kenya kwa siku zote tatu walikuja kutungalia ila najua  Misri wanachohitaji zaidi ni sare ili wafuzu kwa fainali hizi, lakini hawataipata Tanzania,"amesema Mkwasa. Mchezo huo dhidi ya Misri ni mgumu sana ila ana uhakika vijana wake watajitahidi ili kupata matokeo mazuri zaidi.

Amesema wanatarajia kuanza mazoezi kesho huku Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakiratajiwa kuungana na wenzake kwa ajili ya maandalizi ya Jumamosi, huku akitolea ufafanuzi suala la Nadir Haroub 'Canavaro' kutokujiunga na wenzake  hata baada ya kuitwa na kusema hilo lipo nje ya uwezo wake ila ataongea nae atakapopata muda.

Anasema ushindi wa Jumamosi ijayo ni wa kuvuna pointi tatu ili kupata kasi ya kushinda mchezo dhidi ya Nigeria na kufungua ukurasa mpya wa Taifa Stars kutengeneza mazingira mazuri ya kuwashinda Nigeria katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi utakaofanyika Septemba, mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...