Kampuni baba ya saruji, Dangote Cement imepunguza bei ya saruji yake ili kuongeza ushindani kwenye soko la saruji Tanzania. 

Alhaj SadaLadan-Baki, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Dangote amesema bei ya saruji yao aina ya 32.5R imeshuka mpaka kufikia shilingi za kitanzania 10,000 kwa mfuko wa kilo 50 wa saruji, wakati saruji ya 42.5R ikiishuka mpaka shilingi za kitanzania 10,500 kwa mfuko wa kilo 50 kutoka kiwandani mpaka popote uliko hapa Dar es Salaam.

Hatua hii inafanya saruji ya Dangote kuwa ya bei nafuu kuliko saruji zote hapa nchini. Sada amesema hatua hii itasaidia maendeleo ya miundo mbinu na kutilia mkazo mpango wa taifa wa kukabili tatizo la makazi nchini, kitakwimu nchini ina uhaba wa nyumba milioni 3. 

Uwekezaji wa kampuni ya Dangote utatoa mchango mkubwa katika mipango endelevu ya uboreshaji miundo mbinu, kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na kuboresha uchumi kwa ujumla.

“Tunatambua uhitaji mkubwa wa miundo mbinu bora, na moja ya njia ya kulikabili tatizo hili ni kumfanya kila mtanzania kuweza kuwa na uwezo wa kununua rasilimali za ujenzi kwa kuweka bei mbadala kwa kila mtanzania,” alisisitiza. 

Uwekezaji wa zaidi dola za kimarekani milioni 600 utaongeza kasi ya ukuaji na uboreshaji wa miundo mbinu, ajira na kuisaidia serikali katika jitihadi zake za kukuza uchumi wa nchi. Dangote Cement.

Kampuni ya Dangote Cement inajihusisha na utayarishaji, uzalishaji ,utafiti wa kisayansi na ugavi wa saruji na bidhaa nyingine za ujenzi. Kamouni hii iko Nigeria, Benin, Ghana, Congo, Senegal, Tanzania, Afrika ya Kusini na Zambia. Kampuni hii vile vile ndio kamouni inayoongoza kwenye mauzo ya hisa katika soko la hisa la nchini Nigeria.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...