Herieth Paul Mwanamitindo wa Kimataifa anayeishi Jijini New York, Marekani amenyakua tena TUZO ya Mwanamitindo wa Mwaka (MODEL OF THE YEAR 2016) iliyotolewa na (Canadian Annual Art and Fashion Awards (CAFA) katika dhifa iliyofanyika Jijini Toronto, Canada siku ya tarehe 14/4/2016.
TUZO ya mashindano ya Mitindo ya Mwaka ya Canada yenye ushindani mkali hutolewa kwa Mwanamitindo aliyeonyesha kiwango cha juu na aliyetoa mchango mkubwa katika tasnia ya mitindo nchini Canada.
Itakumbukwa kuwa mwezi Februari, 2016 Herieth Paul aliipeperusha bendera ya Taifa na kuitangaza Tanzania duniani kote kwa kuchanguliwa na Kampuni ya Vipodozi ya Kimataifa ya MAYBELLINE INC. ya Jijini New York, Marekani kuwa Balozi na mtangazaji wa vipodozi vyake duniani; akiwa ni Mwanamitindo wa kwanza Afrika Mashariki kupata Heshima hiyo.
Herieth mwenye umri wa miaka ishirini (20) amekuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na vijana nchini Tanzania, kuwa kila jambo linawezekana endapo utamtanguliza Mungu na kufanya kazi kwa bidii zote.




Hongera sana dada na usiogope endelea na kazi na Mungu atakutangulia kama ambavyo wewe mwenyewe uhainisha. Hongera sana.
ReplyDeleteHongera dada kupata tuzo hii.
ReplyDelete