Mkurugenzi Mkuu wa Regency Innovation Solution,  Mike Raymond akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Wakati wa  kusaini mkataba wa maelewano wa kutoa huduma ya kadi ya malipo ya kipekee ya Visa katika bara zima la Afrika wakianzia nchini Tanzania. 
na uzinduzia kadi mpya ya malipo itakayoitwa Mimosa Black Card, kadi ambayo itaruhusu mteja kuweka na kutoa fedha bila ya kuhitaji akaunti ya benki.
amesema kuwa Kadi hii mpya ni sawa na kadi ya kawaida ya malipo ya kabla ila ni ya kipekee kwa sababu haiunganishwi na akaunti ya benki hivyo kuifanya kuwa ya gharama nafuu na pia urahisi wa kuweka na kutoa fedha. Kadi hii pia italindwa kwa neno la siri (PIN) na teknolojia ya juu ya ulinzi.

Watumiaji wa kadi ya Mimosa wanaweza kutoa fedha katika mashine za kutolea fedha (ATM), kufanya malipo ya kutumia kadi katika maeneo yote yenye huduma hiyo na pia kufanya manunuzi mtandaoni mahali popote duniani kupitia mtandao wa Visa. Vile vile wateja wanaweza kuweka pesa katika kadi zao kupitia tawi lolote la UBA Tanzania au mitandao ya simu M-pesa, Tigo Pesa, Airtel Money na pia katika akaunti za kukusanya fedha katika benki za CRDB na Exim. 
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha Philemon akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leoamesema kuwa “ Lengo letu kuu ni kubadilisha mfumo wa jinsi watu wanavyotumia huduma za kibenki haswa kwa kujikita katika kundi la wale ambao hawatumii huduma za benki kwa kupitia teknolojia kama hizi. amesema kuwa ushirikiano wao na Regency Innovation Solutions utafanikisha lengo kwa kuwafikia wale wasiotumia huduma za benki na kuwajumuisha katika huduma hizi katika Tanzania na bara la Afrika. 
Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha za Kielektroniki wa UBA Tanzania, Tesha Philemon na  Mkurugenzi Mkuu wa Regency Innovation Solution,  Mike Raymond  wakibadilishana mikataba leo jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...