Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Taifa Shaka Hamdu Shaka akiwa anaongea na wananchi wa tanga
……………………………………
Na Woinde Shizza,Tanga

Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM )umevitaka vyama vya
upinzani wanaopika maneno ya majungu yenye lengo la kuwagonganisha viongozi wa CCM,Waache kumsumbua sumbua Mwenyekiti wa CCM Dk Jakaya Kikwete astaafu kwa heshima, kwa sababu ameitumikia nchi yake kwa kutoa jasho jingi miaka kumi iliopita, Aidha umoja huo umesisitiza kuwa kazi aliyoifanya Dk Kikwete katika uongozi wake wa miaka kumi kisiasa na kiserikali utabaki kwenye vitabu vya kumbukumbu ya historia iliotukuka, hususan kila utakapokumbukwa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM mwaka 2015.

Kaimu katibu mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo wakati alipozungumza na viongozi na wanachama wa uvccm na ccm kwenye ukumbi wa TANU Hall mjini Tanga.Alisema baada ya upinzani kubaini kukosa hoja na hawakubaliki katika jamii maadui wa kisiasa wanotimiwa na nafisadi wamekuwa wqkijaribu kupika uzushi na kutaka kuionyesha jamii kwamba viongizi wa chama tawala hawana maelewano.

“Nakupeni usia viongozi wa Ukawa ambao sasa mmekuwa wakiwa , mambo ya ngoswe waachieni ngoswe wenyewe, viongozi wa ccm hawagombani, hawajawahi kugombana na kamwe hawatagombana milele “alisema shaka Aliwataka viongozi hao kutazama mustakabali wao kisiasa na kuachana na ccm kwa sababu chama hicho tawala haiwezekani kubomoka kwa maneno ya jikoni , vijiweji au vichochoroni.

Shaka alisisitiza kuwa mwenyekiti wa ccm Dk Kikwete wakati akiwa Rais ameitumikia nchi yake kwa kadri ya uwezo wake kama ambavyo walivyotenda na kuitumikia nchi viongozi watangulizi wake akiwemo baba wa Taifa Mwalimu julius Nyerere, Mzee Ali Hassan Mwinyi, Mzee Benjamin Mkapa na yeye ametenda kwa uwezo wake kama atakavyotenda Rais Dk John Magufuli katika kipindi chake.

“Mtu mwenye akili timamu kila atakaposafiri akiizunguuka nchi yetu na kupita juu ya barabara za lami, ujenzi wa madaraja, kutanuka kwa mawasiliano, kukua uchumi wa Taifa na wa mtu mojmoja na wananchi kiushi katika nyumba za kisasa lazima utamkunbuka Kikwete taka usitake
“alieleza Kaimu huyo katibu mkuu . 

Alisema kila zama ina kitabu na Nabii wake hivyo mema yaliofanywa na kiongozi mmoja aliyemaliza muda wake yanahitaji kuheshimiwa kwa sababu  Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wote ni watoto wa baba na
mama mmoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...