Mkurugenzi wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege akimuelezea jambo Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa.

TIB Corporate Bank imefadhili mkutano mkuu wa bodi ya usajili wa wakandarasi nchini unaotarajiwa kufanyika jijini Mwanza kwenye hoteli ya Malaika kuanzia tarehe 5 hadi 6 mwezi huu wa tano ikifuatiwa na mkutano mwingine utakaofanyika jijini Dar es salaam katika ukumbi wa Daimond Jubilee kuanzia tarehe 26 hadi 27 mwezi huu wa tano. 

Mkutano huo, ambao mwaka huu una kauli mbiu ya ‘Kuwajengea Uwezo Wakandarasi wa Ndani kwa ajili ya Uchumi Endelevu: Changamoto na Mipango ya baadae?, unalenga kuwakutanisha wadau na wakandarasi kujadili mchango wa wakandarasi na ushiriki wao katika kukuza uchumi wa nchi.

Akizungumzia udhamini wa katika mkutano huo, Mkurugenzi wa TIB Corporate Bank, Bwana Frank Nyabundege alisema benki yake inazifahamu changamoto zinazowakabili wakandarasi wengi nchini ikiwemo ukosefu wa fedha ambao unazuia kupanua na kuendeleza uwezo wao wa kushindana katika sekta ya ujenzi hasa katika kupata zabuni na utekelezaji wa mikataba.

TIB Corporate Bank imeweka misingi ya kuhakikisha inatoa huduma bora kwa wateja wake na ndio maana tumeweza kuja na suhulisho kwa ajili ya kuwasaidia wakandarasi kuweza kuendesha shughuli zao kwenye mazingira yao ya kazi’ alisema Bw.Nyabundege.

Bwana Nyabundege pia alisema udhamini wa mkutano wa wakandarasi unalenga kujenga na kuimarisha uwezo wa wakandarasi kupata fursa ya kuendeleza sekta ya ujenzi nchini.TIB Corporate Bank ilianzishwa kwa lengo la kutoa huduma za nyongeza za kibenki kama mtaji wa kufanyia kazi, mikopo pamoja na uwezeshaji wa kibiashara kwa ajili ya wateja mbalimbali kupitia ubunifu wa teknolojia, kukuza thamani kwa wadau na pia kuchangia katika ujenzi wa taifa kwa kutoa huduma mtambuka za kifedha na kuchangia ukuaji wa uchumi shindani sambamba na Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025.

TIB imefanya mabadiliko ya kitaasisi ili kuweza kuwa kituo cha huduma zote za kifedha kwa kushughulikia mahitaji ya wawekezaji wa ndani wote kwa lengo la kusukuma maendeleo ya uchumi wa taifa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...