Wakati
Coastal Union ya Tanga ikiwa imeaga rasmi Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania
2015/16, swali linabaki kwa wadau wa soka nchini kwamba ni timu gani
itaungana na Wagosi wa Kaya kushuka daraja kutokana na timu tano kuwa
katika hatari?
Pazia
la msimu wa Ligi Kuu 2015/16 linatarajiwa kufungwa Jumapili ijayo Mei
22, mwaka huu na timu tano zinazoonekana kuwa katika hatari ya kuungana
na Coastal Union yenye pointi 22 (nafasi ya 16) kushuka daraja. Kati ya
timu hizo tamo, mbili ndizo zitaungana na Coastal kushuka daraja hivyo
kuwa na jumla ya timu tatu.
Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini
SERENGETI
BOYS ANA KWA ANA NA INDIA
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 maarufu
kama Serengeti Boys, Bakari Shime amesema hana wasiwasi kuwavaa
India-wenyeji wa michuano maalumu ya soka ya kimataifa kwa vijana (AIFF
Youth Cup 2016 U-16) yaliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo
(AIFF).
Shime
ambaye kikosi chake kilitoka sare ya 1-1 na Marekani Jumapili ya Mei
15, 2016, kesho Jumanne kikosi chake kitawavaa India kwenye Uwanja wa
Tilak Maidan, Vasco jijini Goa kabla ya kuahidi kuwatungua wenyeji hao
kwenye michuano hiyo inayofanyika ikiwa ni kuipa baraka India kabla ya
fainali za kombe la Dunia kwa vijana mwakani-2017.
Kwa taarifa zaidi fuata link hapo chini
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...