MFUKO wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa kushirikiana na Shirika la Kazi Duniani (ILO) wameanza kutua mafunzo kwa madaktari nchi nzima kuhusu namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yanatosababishwa na kazi. Jumla ya madaktari 380 wa hospitali za rufaa mikoani na wilayani watafaidika na mafunzo hayo.

Mafunzo yatatolewa kwa siku tano katika vituo vikubwa vinne ikiwemo Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya. Wataalamu kutoka ILO waliobobea katika ajali na magonjwa yanayotokana na kazi Dr. Jacques Pelletier na Dr. Sylvie Thibaudeau ndio watakaoendesha mafunzo hayo.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi Bw. Masha Mshomba amesema kwamba mafunzo haya ni hatua muhimu sana kwa Mfuko kwani Mfuko unaanza rasmi ulipaji wa mafao tarehe 01 Julai 2016 kwa Wafanyakazi wote watakaopata ajali au magonjwa kutokana na kazi. Miongoni mwa mafao yataayotolewa ni Huduma ya matibabu, Fidia kwa ulemavu wa muda, Fidia kwa ulemavu wa kudumu, Ukarabati na ushauri nasaha, Malipo kwa anayemhudumia mgonjwa, gharama za mazishi endapo mfanyakazi atafariki na fidia kwa wategemezi endapo mfanyakazi pia atafariki.
Bw. Masha Mshomba akifafanua dhumuni kubwa la kufanya haya mafunzo alisema, “Kazi kubwa ya madaktari hawa itakuwa ni kufanya tathimini ya magonjwa yanayotoka na kazi na kutupa ushauri wa kuendelea na malipo kama wahusika watakuwa wamepata ajali au kuugua na wakapata ulemavu”.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw. Masha Mshomba akielezea malengo ya Mfuko na kazi zake, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano kwa madaktari kwenye jengo la LAPF jijini Dar es Salaam Mei 16, 2016. Mafunzo hayo yanalenga kuwaelimjsha madaktari namna ya kubaini na kushughulikia wahanga wa ajali na magonjwa yatokanayo na kazi.



Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii, SSRA., Bi. Irene Isaka, akitoa hotuba ya ufunguzi.

NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said

Baadhi ya washiriki wa mafnzo wakifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...