Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BARAZA la Michezo la Taifa (BMT) limewatuhumu baadhi ya watendaji wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) kutaka kukwamisha uchaguzi wa Klabu ya Yanga kwani kwa kipindi kirefu klabu hiyo ilikuwa ikitumia uongozi wa zamani baada ya kutofanya uchaguzi wake mkuu kwa muda mrefu sasa.

Kutokana na hali hiyo uongozi mpya wa BMT ulitoa agizo kwa vyama vyote vya michezo ikiwemo klabu za mpira za miguu ikiwemo Yanga kufanya uchaguzi kwa ajili ya kupata viongozi wapya lakini baraza liliitaka Yanga kufanya uchaguzi kabla ya Juni 30 baada ya kuomba kusogezewa mbele tarehe iliyopangwa awali kutokana na kushiriki mechi za kimataifa.

Akizungumzia tuhuma hizo Kaimu Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja amesema kuwa anasikitishwa na baadhi ya watu ikiwemo watendaji wa TFF kutaka kukwamisha zoezi la uchukuaji fomu wa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo lakini kutokana na hali hiyo wangependa wanayanga kujua kuwa uchaguzi upo palepale kama walivyoeleza awali.

"Licha ya baadhi ya watu kutaka kukwamisha mchakato huu lakini tunapenda tu kuwajuza kuwa uchaguzi unatakiwa kufanyika kabla ya Juni 30", amesema Kiganja.

Kwa upande wake Afisa habari wa TFF, Alfred lucas alisema kuwa hadi sasa watu waliojitokeza kuchuakua fomu hizo ni watatu huku mbili zimetolewa kwa watu wanaogombea nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji huku Aron Nyanda akijitokeza kuwania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu hiyo.

"Hadi sasa wamejitokeza kuchukua fomu ni watu watatu  wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Yanga huku zoezi likiwa linaelekea ukingoni", amesema Alfred.

Aidha BMT imetangaza zoezi hilo kumalizika Jumapili badala ya leo kama ilivyotangazwa na TFF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...