Na Zainab Nyamka,Globu ya Jamii.
TIMU ya Taifa ya Wanawake Twiga Stars inatarajia kucheza mechi ya kitaifa ya kirafiki dhidi ya timu ya wanawake ya Rwanda mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 17 katika mji mkuu wa Rwanda, Kigali.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam  leo  Afisa habari wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), Alfred Lucas amesema kuwa Twiga imeshathibitisha kukubali mwaliko huo na katika barua waliyoituma, wameomba mechi hiyo ya kirafiki kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao za fainali za Mataifa ya Afrika kwa upande wa wanawake.

"Wenzetu wameomba mchezo huu kwa ajili ya kuandaa kikosi chao baada ya kufuzu kuelekea katika mashindano fainali za mataifa ya Afrika", amesema Lucas .
Rwanda wameona kuwa kiwango kizuri kilichooneshwa na stars katika mechi zake mbalimbali ikiwemo ile ya kuwania kufuzu kucheza fainali hizo ni kizuri kwa timu yao,"Timu hiyo iliona kiwango kilichooneshwa na Twiga ni kipimo kizuri kwa timu yao kuelekea katika fainali hizo kwa upande wa wanawake", amesema Lucas. K utokana na mechi hiyo Twiga itaingia kambini hivi karibuni kwa ajili ya maandalizi ya kuwavaa Rwanda".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...