JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA NISHATI NA MADINI

 TAARIFA KWA UMMA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. John Pombe Magufuli, amemteua Dkt. Alex L. Kyaruzi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.), amewateua wafuatao kuwa  Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO kuanzia tarehe 31/5/2016 hadi tarehe 30/5/2019;
1.   Dkt. Samwel Nyantahe
2.   Dkt. Lugano Wilson
3.   Bw. David Elias Alal
4.   Mhandisi Stephen Peter Mabada
5.   Mhandisi Leonard R. Masanja

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mb) amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), kuanzia tarehe 30/5/2016 hadi 29/5/2019 wajumbe  hao ni :
  1. Bw. Abdalah H. Musa
  2. Dkt. Coretha Komba
  3. Bw. Felix M. Maagi
  4. Dkt. Lightness Mnzava
  5. Bw. John B. Seka 
Uzinduzi wa Bodi hizo utafanyika Makao Makuu ya Mashiriki hayo Siku ya Alhamisi tarehe 2 Juni, 2016, saa 4:00 asubuhi kwa Bodi ya STAMICO na saa 8:00 mchana kwa Bodi ya TANESCO.

Imetolewa na;
KATIBU MKUU
31 MEI, 2016

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...