kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka hamdu Shaka 

Na Woinde Shizza,Kilimanjaro 

Jumuiya ya vijana UVCCM imetoa wiki moja kwa wale wote waliouza viwanja na rasilimali za jumuiya hiyo kujiandaa kwa ajili ya kupelekwa mahakamani .

Agizo hilo limetolewa na kaimu katibu mkuu wa UVCCM taifa Shaka hamdu Shaka wakati akiongea na viongozi wa umoja huo wakiwemo wenyeviti wa mikoa ,wenyeviti wa wilaya pamoja na makatibu wa umoja huo kutoka katika mikoa ya Arusha ,kilimanjaro pamoja na Manyara waliokutana katika ofisi ya CCM wilaya moshi mjini katika majumuisho ya ziara yake alikuwa akifanya katika mikoa hiyo.

Alisema kuwa baadhi ya watu wamegeuza mali za jumuiya hiyo kama shamba la bibi, kwani kila mtu aliyekuwa akitumia mali hizo na kuzitawanya kama anavyotaka, hivyo atahakikisha anawachukulia hatua kali za kisheria kwa kuwapeleka mahakamani wale wote ambao wamehusika kufanya hivyo.

Alibainisha kuwa kwa sasa hivi katika uongozi wake amezamiria kuimarisha jumuiya hiyo na hatosita kuchukua hatua kwa yeyote yule wala kumuonea huruma yeyote yule ambaye amezifujaa mali hizo za jumuiya kama shamba la bibi.

Pia kwa upande wa utendaji ndani ya Jumuiya hiyo alisema kuwa kwa mtendaji yeyote ambaye anaona hawezi kwenda na mabadiliko na kasi anayoitaka aachie ngazi mapema kabla hajamkuta, maana hatamuonea huruma yeyote kwani hawataki watendaji wavivu wala mizigo ndani ya chama .

Alibainisha kuwa muda wa majungu ,fitina ,umbea na poroja umeisha na sasa ivi kinachohitajika ni mabadiliko ya utekelezaji wa majukumu ya kazi za kila siku, kufuata vikao vya kikanuni na kubuni miradi ya maendeleo na itayokuza uchumi kwani UVCCM anayohitaji kwa sasa ni ya siasa na uchumi huku akiziagiza wilaya zote na mikoa kubuni miradi mbalimbali ya maendeleo. 
Baadhi ya wafuasi wa CCM wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...