Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akizungumza watu wenye ulemavu na wadau wa maendeleo nchini mara baada ya uzinduzi wa kanzidata kwa ajili ya watu wenye ulemavu nchini.
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu Mhe. Dkt Abdallah Possi akifatilia uwasilishwaji wa kanzidata ya watu wenyes ulemavu nchini iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. 
Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO. 

Na Raymond Mushumbusi - MAELEZO
Bwana Joachim Marege ni mtu mwenye ulemavu asiyeweza kutembea. Baba huyu anakofanyia kazi inabidi apande lifti hadi ghorofa ya kumi. Siku moja nikiwa nimeongozana naye kwenye lifti mara ghafla umeme ukakatika. Baada ya lift kufunguliwa nikamsaidia kutoka kwenye lift na kuendelea na safari yangu  lakini kwa ndugu huyu haikuwezekana kuendelea na safari yake kwa kupanda ngazi ilibidi asubiri kwa muda  hadi umeme utakaporudi ndo akapanda lift na kwenda ofisini kwake. Hii ni changamoto sana kwa watu wenye ulemavu katika kupata miundombinu rafiki ya kuwawezesha katika shughuli zao za kila siku na ambao idadi yao inaongezeka kila kukicha.

Mnamo Aprili 11 2016 Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakishirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu walizindua kanzi data maalum kwa ajili ya kupata takwimu za watu wenye ulemavu nchini.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani, zaidi ya watu bilioni moja dunia sawa na asilimia 15 ya watu wote duniani wanakadiriwa kuwa na aina fulani ya ulemavu. Idadi ya watu wenye ulemavu inaongezeka kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo ajali, majanga ya asili na ya kusababishwa na binadamu, ongezeko la watu hasa wenye umri mkubwa, magonjwa ya kuambukiza, magonjwa ya akili na matatizo sugu ya kiafya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...