Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imesikitishwa na tukio la ubakaji na udhalilishwaji lililofanywa na wanaume wawili dhidi ya mwanamke mmoja, ambaye alishurutishwa kuwa mtupu, kufanya ngono bila ridhaa yake, kupigwa picha na kusambazwa katika mitandao ya kijamii hapa nchini.
Wizara inalaani vikali kitendo hiki cha ukatili na udhalilishaji kilichofanywa na wanaume wawili, ambao wamekamatwa na Polisi kwa kuhusishwa na udhalilishaji huo. Mazingira ya ukatili huo yanahuzunisha, kwani inaelezwa kuwa wanaume hao kwa wakati mmoja walihusika kumwingilia kimwili pasipo ridhaa yake, ilihali,wakimpiga picha za tukio zima la ubakaji huo.
Kitendo hiki, ni ukatili usio na kifani, maana kimefedhehesha utu wake binafsi na kudhalilisha familia yake, na wanawake kwa ujumla. Aidha, kitendo hiki kinaweza kusababisha madhara makubwa kwa mwanamke huyukimwili,kisaikolojia, kijamii na kihisia.
hao ni wauwaji. nani anawahitaji kwenye jamii hao? wapewe ile adhabu ya kuwapoteza kabisa. wanaume badilikeni.
ReplyDeleteKitendo walichofanya ni cha kikatili, kinyama na sidhani kama hao wanaume ni binadaamu. Hivi wajiulize, je wangefanyiwa wao hivyo wangejisikiaje? Je ni sawa wangefanyiwa wao hivyo?? Kwa kweli wapewe adhabu kali hata ikibidi kuhukumiwa kifo ili iwe funzo kwa watu wengine wasifanye unyama huu!
ReplyDeleteHizi tabia chafu hazikubaliki kwa nini wahusika wanabaka badala ya kuoa? Haiingii akilini
ReplyDelete