Balozi
wa Tanzania nchini Sweden, Mhe. Dora Msechu amefanya mkutano wa
kifungua kinywa (breakfast meeting) na wafanyabiashara wa Sweden
uoliandaliwa na Baraza la Biashara la Sweden na Afrika
Mashariki(SWEACC). Mhe. Balozi Dora Msechu amewahamasisha
Wafanyabiashara wa Sweden kuwekeza Tanzania kwa kuweleza kwa kina fursa
zilizopo pamoja na juhudi mahsusi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania
kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kukuza uchumi wa nchi
ikiwa ni pamoja na mikakati kabambe ya kuimarisha sekta ya viwanda na
kuboresha miundombinu.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...