Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inakusudia kupanga Miji mingine  Miwili Midogo ya Wete Kisiwani Pemba na ule wa Makunduchi Unguja katika azma yake ya kuhimiza matumizi bora  na ya kudumu  ya ardhi hapa Nchini.
Mipango hiyo itaenda sambamba na kufanya mapitio ya mpango wa maendeleo ya Utalii katika eneo la Pwani ya Mashariki ya Kisiwa cha Unguja  inayoanzia kutoka Chwaka Wilaya ya Kati hadi Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A”.
Akifunga  Mkutano wa Pili wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanmzibar, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba migogoro ya ardhi bado imekuwa changamoto kubwa inayoisumbua Serikali kwa muda mrefu sasa.
Balozi Seif  alionya kwamba Wananchi wengi hawataki kuheshimu Sheria ya Ardhi jambo ambalo linaibuwa migogo ya ardhi kila uchao. Hivyo katika kumaliza au kupunguza migogoro hiyo aliiomba Mahkama ya Ardhi kuzishughulikia Kesi za migogoro ya Ardhi haraka iwezekanavyo.
Akizungumzia tatizo la ajira kwa watoto Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliwanasihi wazazi  kuwacha kuwatumikisha  kazi watoto wao  hasa zile hatarishi kwa kisingizio cha kujiongezea kipato cha familia ili kupunguza tatizo hilo lililolikumba Taifa kwa hivi sasa.
Balozi Seif alisema Familia bado zina jukumu kubwa la kuhakikisha watoto wao wanapata haki zao za msingi ikiwemo elimu na malezi bora kwa lengo la kuwajengea mazingira mazuri ya maisha yao ya baadaye.
Alifahamisha kwamba kuwepo kwa ajira za watoto hapa Zanzibar bado ni suala kubwa na Serikali inaendelea na jitihada za kulitafutia dawa ya kulikomesha kabisa  ili kuendana na sera na miongoizo ya Kimataifa juu ya kuondokana na tatizo hilo sugu.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunga Mkutano wa Pili wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiufunga Mkutano wa Pili wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar uliokuwa ukijadili Bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/2017 katika Ukumbi wa Baraza hilo uliopo Mbweni nje kidogo ya Kusini mwa Mji wa Zanzibar.
 Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kufungwa kwa Baraza la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani.
Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakisikiliza Hotuba ya kufungwa kwa Baraza la Wawakilishi iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hayupo pichani. Picha na  OMPR – ZNZ.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...