Na
Sixmund J. Begashe
Makumbusho
na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam imezindua rasmi program ijulikanayo kama Museum
Arts Explosion ili kutoa nafasi kwa wasanii wa hapa nchini kufanya kazi zao za
sanaa kwenye jumba hilo la Makumbusho ya Taifa kwa malengo ya kuendeleza na
kukuza Sanaa na Utamaduni nchini.
Akipokea
salamu mbali mbali za pongezi kutoka ndani na nje ya nchi baada ya onesho zuri
na lililo sisimu wengi waliofika kuliona kwenye Ukumbi wa Makumbusho hiyo,
Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure ameeleza kuwa,
wadau wengi wamependezwa sana na maamuzi haya ya Makumbusho ya kuinua uhai wa
Sanaa nchini kwa kupitia Programu hii ya sasa.
“Hii ilikuwa ni kiu ya wasanii walio wengi
hapa nchini, kiu ya kuwa na sehemu watakayo oneshea kazi zao wanazo zalisha, na
si kwa wasanii tu pia kwa watazania na wageni mbali mbali kwani walikuwa
wakipata shida sana kuwa na mahali maalumu pakuonea sanaa za jukwaani, lakini
sasa tumesha fungua milango kwa wasanii wote hapa nchini ambao watakuwa
wamejiandaa vizuri kuja kujisaliji ili kuwekwa kwenye program hii mpya”
alisema Bw Bufure.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti Msanii wa Kimataifa
Bw Isack Abeneko na Bw Aloyce Makonde wameipongeza Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni
kwa kuwapa heshma ya kuizindua program hio kwa wao kufanya onesho lakwanza na
lililo onesha mafanikio makubwa kwa kuudhuriwa na watu wengi, hivyo wametoa
wito kwa wasanii hapa nchini kuitumia nafasi hii adhimu ili kuifikishia adhira
Mafundisho, Maonyo na Burudani kama yalivyo matarajio yao.
Mratibu
wa Program hiyo Bw Edgar Chatanda ameielezea program hiyo kuwa kwa sasa itakuwa
ikiandaa maonesho kila Ijumaa ya mwisho
wa Mwezi ili kutoa nafasi kwa menejimenti ya Program kujidhirisha na ubora wa
onesho kabla ya kupandishwa jukwaani, pia kupata muda wa kutosha wa kufikisha
taarifa ya onesho hilo kwa umma ili watanzania wapate hii haki ya kuona kazi za
wasanii wa hapa nchini.
“Program hii ni endelevu, na tutakuwa na aina
mbali mbali za kazi za sanaa zitakazo oneshwa hapa Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni, tulikuwa na wasanii wa Dance Garage chini ya wasanii wa kimataifa,
kwa kweli walifanya vizuri sana, onesho linalofuata litakuwa tarehe 29 Julai
2016 litakalo fanywa na Mwanamuziki wa Kimataifa wa Rege pamoja na Wasanii wa
ngoma za ubunifu wa MUDA AFRICA, hivyo nitoe wote kwa watanzania kujitokeza kwa
wingi kwenye maonesho haya kwani onesho lililopita wageni kutoka nje na watu
maarufu tu ndio walio uduria”. Alisema Bw Chatanda.
Msanii wa Kimataifa Bw Aloyce Makonde a.k.a
Mkulima akionesha ubunifu wake wa dance alioiita MSOMI MAKOLOLI ionesha kwenye
onesho la Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es
Salaam.
Hapo si barabarani bali ni jukwaani, wasanii
wa ngoma za ubunifu Bw Tiko Mbepo alie simama kulia na Bw Isack Abeneko alieko
juu ya Pikipiki wakimaliza onesho kwa kuwaacha jukwaani baadhi ya adhira walio
ichukuwa na kuiweka jukwaani kama sehemu ya onesho lililofanyika kwenye Jukwa
la Maonesho la Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
Pichani haya si masumbwi ya kweli bali ni
sehemu ya ngoma ya ubunifu iliyo itwa MACHO MATATU ikichezwa na wasanii wa
ngoma za ubunifu Bw Tiko Mbepo alie kushoto na Bw Isack Abeneko kulia kweye
onesho la Museum Arts Explosion kwenye Jukwa la Maonesho la Makumbusho na
Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaama.
Wasanii wa kikundi cha DDI wakiwa onesha umahiri
wao kwenye ngoma ya ubinifu ijulikanayo kama Freedom (Uhuru) iliyo waliyo
ionesha kwenye onesho la Museum Arts Explosion, Makumbusho na Nyumba ya
Utamaduni Dar es Salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...