Wafanyakazi
wa benki ya Exim, wateja pamoja na watu wengine Tanzania jana
walijotokeza kwa wingi kwenye makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es
Salaam kwa ajili ya kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku
ya uchangiaji damu duniani.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati zoezi hilo likiendelea, Mkuu wa kitengo cha Rasilimali watu kutoka benki hiyo Bw. Frederick Kanga alisema hatua hiyo ni muendelezo tu kwa kuwa kuwa wamekuwa wakifanya hivyo tangu mwaka 2010 na lengo kuu kukabiliana na tatizo upungufu wa damu salama kwenye vituo vya afya hapa nchini.
“Mara zote tumekuwa tukijisikia kuwa na furaha ya ajabu inapofika siku kama hii ya leo kwa kuwa tunaamini kwamba tunapata fursa ya kutimiza wajibu wetu kama sehemu ya jamii lakini pia kwa kufanya hivyo tunakuwa tumeshiriki kuokoa maisha ya wenzetu wanaopoteza maisha kwa kukosa damu salama pale wanapoihitaji,’’ alisema.
Kauli hiyo ya Bw. Kanga inakwenda sambamba na kauli mbiu ya uchangiaji damu ya mwaka huu inayosema: “Sote tunaunganishwa na damu’’. Kauli mbiu hiyo inalenga kuonyesha namna gani maisha ya watu wenye uhitaji wa damu huokolewa na wenzao wanaojitokeza kuchangia damu.
Akizungumza wakati akisimamia zoezi hilo Afisa Uhamasishaji na elimu kwa umma kutoka Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bi. Fatma Mujungu alisema uhaba wa damu hapa nchini umekuwa ukichangiwa kwa kiasi kikubwa na mtazamo wa Wananchi walio wengi kwamba wapo tayari kuchangia damu pale tu inapohitajiwa na mmoja wa wanandugu wa familia husika.
“Hivyo basi natoa wito kwa Wananchi mmoja mmoja pamoja na taasisi nyingine kuiga mfano wa benki ya Exim Tanzania ambayo imekuwa na utamaduni wa kuchangia damu kila mwaka ili kuokoa maisha ya watanzania wote,’’ alisema.
Kwa upande mwingine baadhi ya wafanyakazi na wachangiaji hao walisema wamekuwa wakiguswa na hitaji hilo muhimu la kuchangia damu kila mwaka kwa kuwa wao ni sehemu ya jamii na wanahitaji kuleta mabadiliko ndani ya jamii kwa kuokoa maisha ya wenzao wenye uhitaji wa huduma hiyo muhimu.

Mkuu wa Hazina wa Benki ya Exim Tanzania,Bw George Sumbusho (kulia) pamoja na Mkuu wa kitengo Huduma za Reja reja wabenki hiyo Bw Rahul Singh (wa pili kulia) wakichangia damu sambamba na wafanyakazi wenzao waliojitokeza makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani .Anaewahudumia ni Ofisa wa Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bw. Allen Ligonga.

Meneja Msaidizi Huduma kwa wateja wa Benki ya Exim Tanzania, Bw Ally Mandai (kulia) akichangia damu sambamba na wafanyakazi wenzake waliojitokeza makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani .Anaewahudumia ni Ofisa wa Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bw. Allen Ligonga.
Baadhi ya wafanyakazi na wateja wa Benki ya Exim Tanzania waliojitokeza makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam juzi kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu duniani .Anaewahudumia ni Ofisa wa Mpango wa taifa wa damu salama (NBTS) Bw. Allen Ligonga.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...