KLABU
ya Simba SC imekamilisha Usajili wa kiungo mahiri wa Mtibwa Sugar,
Mzamiru Yassin kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia timu hiyo
kuanzia Msimu wa 2016/2017. Mzamiru mwenye uwezo wa kupiga pasi za
uhakika na anaungana na viungo wengine kwenda kuisaidia klabh hiyo
kuweza kufanya vizuri msimu ujao.
"Ni
kweli tulikuwa kwenye mazungumzo na Simba ila kwa sasa kila kitu kipo
vizuri, nimesha saini nao mkataba wa miaka miwili kuweza kuitumikia
klabu hiyo na kushirikiana vizuri na wachezaji wengine ntakaowakuta," .
Amesema Mzamiru.
Simba
wameweza kupata saini ya mchezaji huyo ambaye atakuja kuongeza nguvu
safu ya kiungo ambapo imeonekana wachezaji wake wengi wanashindwa
kusaidiana na safu ya ushambuliaji kwenye kutengeneza nafasi za magoli.
Mzamiru
anakuwa ni mchezaji wa tatu kuondoka kwenye kikosi cha Mtibwa na ni
pigo ligine hasa baada ya mlinzi wa kati Andrew Vicent 'Dante'
kusajiliwa na Yanga sc, huku kukiwa na tetesi za Simba kuwataka Mohamed
Ibrahim na Shiza Kichuya ambao wote wanaichezea timu ya Taifa ya soka ya
Tanzania, Taifa Stars.
Huyu
anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na Simba baada ya Emmanuel Simwanza
kutoka Mwadui na Jamal Simba Mnyate kutoka Mwadui na wakiwa wanafanya
usajili kimya kimya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...