Na Lilian Lundo – MAELEZO - DODOMA
Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha bajeti ya shilingi Trilioni 29.5 ya mwaka wa fedha 2016/17 ambayo iliwasilishwa na Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango June 08, 2016.
Bajeti hiyo ilipigiwa kura na wabunge waliokuwepo bungeni, ambapo jumla ya wabunge 251 walipiga kura za ndio za kuipitisha bajeti hiyo kati ya wabunge 252 waliokuwepo ukumbini wakati  kura hizo zikipigwa.
Katika kupiga kura  Hakukuwa na kura yoyote ya hapana au kutokuamua kati ya wabunge waliopiga kura. Jumla ya wabunge 137 hawakuwepo wakati kura zinapigwa.
  “Naipongeza Serikali kwa kutoa hoja ya bajeti ya Serikali ya mwaka 2016/17 na kupitishwa  na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, namtakia Waziri wa Fedha kila la heri katika hatua zinazofuata katika utekelezaji wa bajezi hii,” alisema Naibu Spika Mhe. Dkt. Tulia Ackson.
Aidha bunge hilo, lilipitisha muswada wa sheria za Serikali kuidhinisha Trilioni 29.5 kwa matumizi ya Serikali kutoka mfuko wa hazina kwa mwaka unaoishia June 30, 2016.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Mpango  amewataka watanzania kulipa kodi na wale wote wanaotakiwa kusimamia ukusanyaji wa kufanya kazi hiyo kwa ukamilifu ili fedha zilizopitishwa katika bajeti ya mwaka 2016/17.
Sheria hiyo ya bajeti ya mwaka 2016/17 inasubiri kusainiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo utekelezaji wake utaanza Julai 01, 2017.
 Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifanya majumuisho leo mjini Dodoma kabla ya kupitishwa kwa kishindo bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
  Wabunge wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifanya majumuisho leo mjini Dodoma kabla ya kupitishwa kwa kishindo bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
 Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson na watendaji wakuu wa bungu wakimsikiliza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akifanya majumuisho leo mjini Dodoma kabla ya kupitishwa kwa kishindo bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2016/17.
 Mawaziri  na Wabunge wakimpongeza  Waziri wa Fedha  na Mipango Dkt. Philip Mpango  pamoja na Naibu Waziri wake Dkt. Ashatu Kijaju mara baada ya kupitishwa kwa bajeti Kuu ya Serikali ya Trilioni 29.5 kwa mwaka wa fedha 2016/17 leo Bungeni mjini Dodoma.
Waziri wa fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango watano kutoka kushoto akiwa na baadhi ya watendaji wa Wizara ya fedha na Mipango  nje ya ukumbi wa Bunge mara baada ya kupitishwa kwa bajeti Kuu ya Serikali, leo mjini Dodoma. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...