Na Lilian Lundo –Maelezo.
HALMASHAURI ya Mji wa Kibaha imeeleza kuwa upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi  wa mji huo kwa sasa  ni asilimia 56 kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na Halmashauri hiyo.

Akiongea kwa njia ya simu Afisa Habari wa Halmashauri hiyo Bw. Innocent Byarugaba amesema kuwa Halmashauri ina jumla ya miradi 11 ya maji ambayo mitano imekamilika na sita iliyobaki iko katika hatua za mwisho.

“Maji safi na salama yanapatikana kwa asilimia 56 ikiwa ni juhudi za Halmashauri za kukabiliana na tatizo la maji na mpaka sasa miradi mitano imekamilika ambayo hutoa huduma ya maji kwa wananchi,” alisema Bw. Byarugaba.

Katika kuhakikisha huduma ya upatikanaji wa maji unakuwa bora zaidi, Byarugaba amesema kuwa jitihada za kukamilisha upatikanaji wa maji unafikia asilimia 100 ambapo wanaendelea kukamilisha miradi mbalimbali inayofanywa na Halmashauri hiyo.

Aliongeza kwa kutaja miradi iliyokamilika kuwa ni pamoja na Mradi wa maji Mtaa wa kwa mfipa Galagaza kata ya Msangani, Vikawe kata ya Pangani, Sagale kata ya Viziwaziwa, Zojosa kata ya Misugusugu na Mwanalugali kata ya Tumbi.

Aidha alianisha miradi mingine ya maji inayotegemewa kukamilika kwa mwaka wa fedha 2016/17 kuwa ni mtaa wa Sofu kata ya Sofu, Muheza kata ya Mailimoja, Kibenge kata ya Msangani, Kibugalo kata ya Visiga, Kalabaka kata ya Misugusugu na Mikongeni kata ya Viziwaziwa.

Bw. Byarugaba alitoa wito kwa kuwataka wananchi kuwafichua watu wanaokata mabomba ya maji na kujiunganishia maji kinyemela kwani kwa kufanya hivyo kunapunguza kasi ya maji na kusababisha watu wengine kukosa maji.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 10, 2016

    Juhudi za kuongeza upatikanaji wa maji safi na salama ziendelee baada ya zaidi ya miaka hamsini ya uhuru nchi hii yenye vyanzo vingi vya maji, mvua ya kutosha, na wataalamu katika fani ya maji inapashwa kuwa mbali katika hili.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...