Na Bashir Yakub.

Suala la wapi ukufungue kesi ni suala kitaalam. Unapokosea mahali pa kufungua kesi unakaribisha kushindwa kesi hata kama una haki katika kile unachodai. Si kila mahakama unaweza kufungua kesi. Zipo mahakama unaweza kufungua kesi na zipo Mahakama huwezi kufungua kesi.

1.MADHARA YA KUFUNGUA KESI MAHAKAMA ISIYO.

Sheria iko wazi kuwa yeyote anayefungua kesi katika mahakama ambayo hakutakiwa kufungua basi kesi hiyo ni sharti itupwe(strike out). Haijalishi una haki za msingi katika madai yako au lah, kitendo cha kufungua pale pasipo stahili chatosha kabisa kufuta kesi yako mara moja.

Kwa madhara kama hayo upo umuhimu mkubwa wa kujua ni wapi pa kufungua kesi na ni mahakama ipi ni sahihi katika lalamiko ulilonalo. Kila lalamiko au shauri linayo mahakama yake sahihi unapoweza kulifungua .

Kuna lalamiko unaweza kufungua mahakama A lakini huwezi kufungua mahakama B. Yapo mambo ya kujua na kuzingatia unapotaka kufungua kesi katika mahakama sahihi.

2..MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUFUNGUA KESI KATIKA MAHAKAMA SAHIHI.

Kwanza ujue eneo ulipotokea mgogoro kuna mahakama zipi. Karibia kila eneo linazo mahakama zake za mwanzo, za wilaya, na za ardhi. Kwa mfano sinza kuna mahakama ya mwanzo Sinza na kuna mahakama ya wilaya ya kinondoni na mabaraza mengine ya ardhi.

Pili ujue kiasi cha thamani ya mgogoro wako. Kwa mfano kama unamdai mtu hela, au fidia, ujue kwa pamoja ukijumlisha zinakuja kiasi gani. Au kama ni mgogoro unaohusu mali basi lazima ujue mali hiyo ina thamani kiasi gani kifedha.

Tatu lazima ujue aina ya mgogoro wako. Kwa mfano je ni mgogoro wa kazi, ni mgogoro wa ardhi, ni mgogoro wa watoto, ni mgogoro /kosa la jinai, ni mgogoro wa biashara au madai mengineyo kama ya fidia, ni mgogoro unaohusu mila na sheria za kiislamu n.k.

Haya yote matatu yatakupa majibu sahihi wapi ukafungue shauri ili kuepuka kufutiwa kesi na kupoteza madai yako ya msingi. Hapa chini tutaona mambo hayo matatu yanavyohusika katika kupata mahali sahihi pa kufungua kesi.

KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...