Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
BAADA ya kutokutumia jezi zenye mdhamini wao bia ya Kilimanjaro, Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) limetolea ufafanuzi kuhusiana na suala hilo kwani kutokana na kanuni za michuano ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa timu yoyote inapoingia kwenye hatua ya makundi (nane bora) haki za udhamini za timu zote zinahamia kwa shirikisho hilo kwahiyo wadhamini wote wanatakiwa kuingia makubaliano na CAF na sio klabu tena.
Afisa habari wa TFF, Alfred Lucas amefafanua hayo mapema leo na kusema kuwa Yanga hawakwenda kwenye vikao vya awali vya timu zilizoingia kwenye hatua ya makundi na ndiyo maana hawakulifahamu hilo ila kwa sasa kama mdhamini atataka aendelee kuweka nembo atatakiwa kukaa chini na CAF na kukubaliana. “Timu yoyote ikifika hatua ya makundi haki za udhamini zote zinahamia kwa CAF, na zaidi Yanga wanaweza kuendelea kutumia jezi zao mpya kama Bia ya Kilimanjaro hawatataka kuweka nembo yao tena.”
Kwa upande wa klabu ya Yanga, Mkuu wa kitengo cha Haabari na Mawasiliano Jerry Muro amesema kuwa mkataba wao na Bia ya Kilimanjaro unaelekea ukingoni kwaniyo ni uamuzi wao kutaka kuendelea nao au kuangalia uwezekano wa kupata kampuni nyingine itakayokuwa na maslahi zaidi na itakayonufaisha klabu yao.
Amesema wakati wanaenda nchini Algeria hawakuwa wanafahamu kuwa kama kuna mabadiliko ya jezi kwani hawakwenda kwenye kikao cha awali cha timu zilizoingia kwenye hatua ya makundi.”
Mpaka sasa yameshajitokeza makampuni mengi sana na zaidi bado wapo kwenye mazungumzo na masuala yote yakia yamekamilika basi atawataarifu mashabiki na wanachama wa Yanga kuhusiana na ujio mpya wa mdhamini.
Yanga kwa sasa watatumia jezi hizo kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na lina uwezekano wa kuzitumia mpaka kwenye ligi kuu msimu ujao. Jezi hizo kutoka kampuni ya Macron zinazotengenezwa nchini Italy limeingia mkataba na Yanga wa kuwavalisha kuanzia sasa huku ikiwa inawavalisha mabingwa wa kihistoria Afrika Zamaleck ya nchini Misri.
Muro amesema, wanataka kuwa tofauti na wengine kuanzia mavazi hado utofauti wa kuendesha timu yao kwani hadi sasa wao ndiyo wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki na Kati na wanataka kuhakikisha wanafika mbali zaidi na kuweka historia nchini. Ukiachilia mbali hilo amewataka mashabiki wa Yanga kuendelea kuisapoti timu yao kuelekea mchezo wao wa pili dhidi ya Tp Mazembe utakaopigwa Juni 28 Jijini Dar es salaam.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...