Kama mojawapo ya makampuni ya Afrika yanayoongoza katika sekta ya burudani za video, MultiChoice inatambua kwamba rasilimali watu ni kitovu cha simulizi ya mafanikio yake-ndio maana inawekeza sana katika kutafuta, kuendeleza na kunoa watu bora kabisa katika sekta. 

Kama kampuni ya kimataifa, falsafa yetu ya kufikiri kimataifa na kutenda kwa ndani ya nchi inaungwa mkono na programu za kuendeleza utendaji wenye nguvu na sera ambazo zimejizatiti katika kuendeleza biashara za ndani na kuajiri watu kutoka miongoni mwa vipaji vilivyolelewa na kukulia nchini. 

MultiChoice Tanzania inayo furaha kutangaza uteuzi wa Bw. Maharage Ally Chande (pichani) kama Mkurugenzi Mtendaji mpya wa MultiChoice Tanzania. 

Chande anajiunga na familia ya MultiChoice baada ya hapo awali kushika wadhifa wa Mkurugenzi Wa Huduma Za Taasisi katika Ofisi Ya Rais-Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Miradi ( President’s Delivery Bureau).

Mwenyekiti wa MultiChoice Tanzania, Bw.Ami Mpungwe, akiidhinisha uteuzi huo amesema; “MultiChoice Tanzania inaona fahari kuhusu uteuzi huu- hakuna shaka kwamba Bw.Chande ni miongoni mwa watanzania watendaji bora kabisa na anakuja pamoja na uzoefu mkubwa katika masuala ya usimamizi  wa taasisi. 

Sifa zake kama mtaalamu wa huduma za kibenki na kifedha pamoja na tekinolojia ya Habari na Mawasiliano ni ujuzi tunaouhitaji katika biashara yetu ili kuipeleka biashara ya Tanzania katika viwango vipya vya hali ya juu. 

Tunamtakia kila la kheri katika majukumu yake mapya na bila shaka atawahudumia wateja wetu wa DStv kwa nguvu na juhudi mpya.” Bw.Chande ni mtanzania wa kwanza kushika wadhifa huu wa juu MultiChoice Tanzania.

Maharage amewahi kushika nyadhifa mbalimbali za kiutendaji kama Afisa Mtendaji Mkuu katika Benki Ya Taifa Ya Biashara(National Bank Of Commerce) kampuni tanzu ya Barclays/ABSA-na pia kutekeleza majukumu ya Meneja Mtendaji wa Tekinolojia na Mawasiliano, Data na Huduma za Ongezeko la Thamani. 

Ana shahada ya Sayansi katika Elektroniki na Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu Cha Dar-es-salaam na Shahada ya Uzamili katika Uongozi wa Biashara kutoka Chuo Kikuu Cha Afrika Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...