Na Zainab Nyamka,Blog ya Jamii

MSHAMBULIAJI wa timu ya Mtibwa Shiza Kichuya amesema bado ana mkataba wa mwaka mmoja kwahiyo watakaomuhutaji wafuate uongozi na wakae mezani kwani yeye hana mamlaka ya kuongea na timu yoyote kwa sasa zaidi kama watakaomtaka wakifikiana makubaliàno hatakuwa na budi kwenda.

Kichuya amesema, kwa sasa haangalii ni timu gani inamuhitaji ila anachokiwaza ni kuweza kujiandaa vyema kuelekea msimu ujao na zaidi anachokifanya kwa sasa ni kufanya mazoezi na toka Jumatatu baada ya kurejea toka kwenye majukumu ya Timu ya Taifa.

"Kama kuna timu inayotaka huduma yangu mimi siwezi kuongea nao kwani bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa na zaidi kwa atakayenihitaji aje kuongea na kiongozi wangu na mimi sitakataa kama wao wakiamua,"amesema Kichuya. Kwa kweli sina mipango ni kuja kufanya mara mbili zaidi ya msimu uliopita kwani nachokijua mimi ni mchezaji na mpira ndiyo kazi yangu kwahiyo najipanga kwa kujikita muda wote kwenye mazoezi.

Kichuya amekuwa moja ya chipukizi wanaofanya vizuri kwenye kandanda na zaidi ameweza kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa na amecheza kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya na kuweza kufanya vizuri.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...