MKOA wa Morogoro upo mbioni kukuza uchumi wake kutokana na kuanza kuchimba madini ya Graphite kwakuwa yampepatikana katika mkoa huo katika kijiji cha Epanko Wilayani Ulanga mkoani humo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe wakati akizungumza na wahariri na waandishi wa andamizi wa vyombo mbalimbali vya habari katika mkutano ulifanyika katika ukumbi wa mikotano wa chuo cha VETA mjini Morogoro leo.
Madini hayo yalipatikana katika matokeo ya tafiti mbalimbali na utafutaji wa madini ambapo madini mengine ya aina mbalimbali yakiwemo ya rubby, spinal, dhahahu, mawe meusi na graphite (kinywe-Pichani Kushoto) yamepatikana katika mkoa huo.
Upatikanaji wa madini hayo utaongeza uwekezaji katika sekta ya madini katika wilaya ya Ulanga utasaidia kukuza uchumi wa ndani na nje utakaotokana na mauzo ya vito kwa kutumia fedha za ndani na za kigeni.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Kebwe Steven Kebwe akizungumza na waandishi wa habari mjini Morogoro leo, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa mwaka wa hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri pamoja na waandishi wa andamizi nchini.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayub Rioba Chacha na Mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Wizara ya Maliasili na Uatalii na Profesa wa masoko na utalii chuo wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, Wineaster Anderson wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini.
Baadhi ya wahariri na waandishi wa habari wandamizi wakiwa katika mkutano wa Mwaka wa Hifadhi za Taifa Tanzania na wahariri na waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini. Mkutano unaofanyika mkoani Morogoro leo.
Picha na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...