Na Zainab Nyamka,Blogu ya Jamii
HATIMAYE tiketi za mechi ya kufuzu mataifa Afrika 2017 (AFCON) kati ya Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) a Egypt unaopigwa kesho katika dimba la Taifa zimeanza kuuzwa asubuhi ya leo huku kiingilio cha Chini kikiwa ni buku tano kwa viti vya Orange,kijani na Bulu na VIP B&C ikiwa ni 10,000.
Mechi hiyo itapigwa majira ya saa 10 jioni na mchezo utakuwa wa ushindani mkubwa ukipelekea Misri wanahitaji sare ili kujiweka kwenye hatua ya kufuzu nayo Taifa Stars ikihitaji ushindi wa goli tatu na zaidi kufufua matumaini ya kuingia AFCON 2017.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...