Na Chalila Kibuda, Globu Jamii

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewataka wenyeviti wa serikali za mitaa kushirikiana na wenye nyumba kuhakikisha wapangaji katika nyumba wanaingia makubaliano ya mkataba na kuwa na picha zao.
Hatua hiyo imetokana na kuwepo kwa watu wanaofanya uhalifu katika maeneo mbalimbali na kushindwa kupatikana pindi polisi wafanyapo operesheni kutokana na kupanga kwenye nyumba hizo lakini wakati akiondoka hawaagi na wenye nyumba wanakosa kuwa na taarifa za watu katika nyumba zao.

Akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam leo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishina (CP), Simon Sirro amesema kuwa wenye nyumba ambao watashindwa kufanya mkataba bila picha likitokea tukio dhidi ya mpangaji msalaba utamuangukia mwenye nyumba kuhusika katika uhalifu uliofanywa.

Wakati huo Jeshi la Polisi linamshirikia Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ), MT 66807 SGT, George Kwisema kwa tuhuma za kukutwa na vipande kumi vya meno ya tembo vyenye thamani ya Sh. milioni 198 vikiwa katika gari yake yenye namba za usajili T.477 AXS aina ya Suzuki Vitara.

Katika tuhuma za vipande vya meno ya tembo wanaoshikiriwa wengine, ni Shafi Muhibu pamoja na Asha Hassan ambao walikutwa katika gari iliyokuwa imebeba meno ya tembo.

Wakati huo huo, Jeshi la Polisi linawashikiria watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na sukari mifuko 35 ya Kilogram 50 ambao walikamatwa Chadibwa Mtaa wa Magogoni Kigamboni Mei 31 mwaka huu, ambayo ilikuwa haijalipiwa ushuru na waliokamatwa na tuhuma za sukari ni Said Bakari (25), Mkazi wa Mbagala , Hamadi Selemani pamoja na Bakari Masudi.

Jeshi la Polisi linafanya upelelezi pia wa mtuhumiwa wa aliyewaleta wahamiaji Haramu na kutoweka katika mazingira ya utatanishi akiwa chini ya ulinzi wa Polisi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...