Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akiongea na wageni waalikwa (hawapo pichani) katika maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda mwaka 1994, maadhimisho hayo yaliandaliwa na Ubalozi wa Rwanda nchini Tanzania na kufanyika leo katika Ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake alitoa wito kwa mataifa yote kuweka mbele suala la amani ili kuepuka kupoteza maisha ya wananchi wasio na hatia ambao ni nguvu kazi ya Taifa katika kujiletea maendeleo.
Balozi wa wa Rwanda nchini Mhe. Eugene Kayihura akiongea na wageni katika mkutano huo, ambapo aliwasihi jumuiya za wanyarwanda popote ulimwenguni kuzidi kuwafariji wahanga wa mauaji hayo na kuzidi kudumumisha amani. 
Kutoka kulia Waziri Mahiga pamoja na Mhe. Balozi Kayihura, Mhe. Alvaro Rogrigues Mwakilishi mkazi wa  Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP) na Bw. Jean Pierre Nkuranga (Mhanga wa Mauaji hayo ya Kimbari), wakiwa wameshika mishumaa iliyowashwa ikiwa ni alama ya matumaini ya maisha ya baadae kwa Wanyarwanda. 
Sehemu ya wageni walioshiriki maadhimisho wakiwemo mabalozi wa mataifa mbalimbali wanaowakilisha mataifa yao nchini, wakuu wa mashirika ya kimataifa wanaowakilisha nchini Tanzania na wageni wengine walikwa wakiwa wameshika mishumaa katika kuadhimisha kumbukumbu hiyo. Kwa taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...