Mbuni anayepatikana Africa na hasa Afrika Mashariki ndiye ndege mrefu na mkubwa kuliko wote duniani na anakadiriwa kufikia urefu wa futi 9 na uzito wa kilo 156. 

1. Uzito mkubwa wa mbuni upo kwenye miguu yake ambayo ndiyo silaha yake kubwa dhidi ya maadui zake. Yasemekana teke moja la Mbuni laweza kumuua BINADAMU NA hata Simba...

2. Mbuni wana Matumbo matatu.........

3. Mbuni ndiye ndege mwenye kasi kuliko ndege wote ama hata wanyama wenye miguu miwili, Kasi ya Mbuni ni Km 70 kwa saa na HATUA MOJA YA MBUNI inaweza kufika hata m5. Mbuni ana Kasi Kuliko hata Farasi. 

4. Yai la Mbuni ndilo kubwa kabisa kupita mayai ya ndege wote likiwa na urefu wa sm15. Uzito wa Yai moja la mbuni ni sawa na uzito wa dazani mbili za mayai ya kuku. Yai hili pia ni gumu kiasi kwamba unaweza kusimama juu yake. 

Uzito wa yai la ndege huyu ni takribani kg. 1.4 ambao ni zaidi ya mara ishirini ya uzito wa yai la kuku na ili kupika yai la mbuni hadi lichemke inachukua zaidi ya saa moja. Kadhalika Mayai ya mbuni huatamiwa kwa muda wa siku 42 hadi kutotolewa vifaranga na kwa wastani mbuni hutaga mayai kati ya 40 hadi 100 kwa mwaka.

5. Manyoya ya mbuni yana historia ya kusisimua sana kwasababu hapo zamani katika dola ya Misri ya kale yalikua yakitumika kama alama ya haki na kwa kipindi cha sasa yamekua yakitumiwa na wataalam wa mavazi kwa ajili ya kuweka nakshi kwenye mitindo mbalimbali ya mavazi.

6. Jicho la mbuni kenye sm5 ndilo Jicho kubwa kuliko wanyama wote duniani likimsaidia kuweza kuona mbali na hasa maadui zake. Jicho la Mbuni ni Kubwa kuliko hata Ubongo wake 

7. Mbuni hawana meno hivyo hutegemea sana mawe kusagia vyakula vyao. Mbuni hakosi kutembea na mawe popote unapomkuta na yasemekana si chini ya Kg1

8. Dume la Mbuni Linangurumo kama za SIMBA.

9. Wanahistoria wengi wanaamini kuwa mbuni wamekua wakiwindwa tangu maelfu ya miaka ya zamani sio kwasababu ya nyama tu, bali pia kwa uzuri wa manyoya unaovutia sana. Tahadhari ni kwamba Usicheze kabisa na mbuni kwenye anga za yai lake.

​10. MBUNI ni ndege mwenye ushirikiano zaidi ya binadamu hasa katika kipindi cha kuatamia mayai mbuni hugawana majukumu ambako jike huatamia wakati wa mchana na dume huatamia wakati wa usiku

11. ​Mguu wa mbuni una vidole viwili  vyenye kucha kwa mbele na kidole cha nje huwa hakina kucha wakati ndege wengine huwa na vidole vitatu hadi vine na uwepo wa vidole hivi humsaidia kuwa na mwendo kasi wa ajabu sana kuliko ndege wengine duniani. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2016

    ASANTE SANA KWA TAARIFA HIIKUHUSU MBUNI. JAMANI WATANZANIA MUNGU AMETUBARIKI NA VINGI TUVITUNZE NA KUVILINDA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...