Tende ni tunda ambalo linaongoza kwa kuliwa sana katika kipindi cha mfungo ndiyo tunda linalolika sana pengine kuliko tunda lingine. Wanasayansi wa masuala ya vyakula wameishafanyia utafiti tunda hili na kugundua kwamba sifa yake kubwa ni kuwa chanzo kikubwa cha virutubisho na nishati ya mwili (energy). Mtu ukila tende mwili huweza kupata nguvu mara moja.
Hivyo ni wazi kwamba waumini wanaofunga mchana kutwa wanahitaji kula vyakula vya kurejesha virutubisho na nishati mwilini ambayo ilikosekana kwa siku nzima. Kutokana na kuwa na kiwango kikubwa cha nishati, mtu anaweza kuendelea kuishi kwa kula tende na maji tu.
Miongoni mwa faida nyingine ni hizi zifuatazo:
Ulaji wa tendo humsaidia sana mhusika kupata kiasi cha kutosha cha protini na vitamin B1, B2, B3, B5, A1, na C, virutubisho ambavyo ni muhimu kwa ustawi wa afya ya mwili.
Pia ulaji wa tende huimarisha na kuboresha mfumo wa usagaji wa chakula tumboni, hivyo kumsaidia mhusika kuondokana na matatizo ya ukosefu wa choo, au matatizo ya kupata choo kigumu kinachosababisha maumivu wakati wa kujisaidia. Imeelezwa na wataalamu kuwa tende ina kiwango kikubwa cha kamba-lishe (fibre) ambazo ni muhimu kwa ulainishaji wa chakula na kuwezesha kupatikana kwa choo kirahisi. Kama una tatizo sugu na la muda mrefu la ukosefu wa choo, tumia tende kama dawa ya kulainisha choo (laxative) kwa kuloweka kwenye maji usiku kucha, kisha asubuhi zikoroge katika maji hayo na kunywa juisi yake, fanya hivyo kwa wiki mara mbili.

Tende pia husaidia kuupatia nguvu mwili na kukuondoa uchovu, hii ni kwa sababu tende ina virutubisho vya sukari asilia kama vile ‘glucose’, ‘sucrose’ na ‘fructose’.
Hali kadhalika tende ina madini aina ya ‘potassium’ na kiasi kidogo cha chumvi (sodium). Madini hayo husaidia kuimarisha mishipa ya fahamu.
Pamoja na hayo tende pia huwasaidia wale wenye matatizo ya ugonjwa wa anemia, (kupungukiwa damu) wanapotumia tende huweza kupata ahueni kwa kula tende kwa wingi.
Mbali na hayo inaelezwa kuwa matumizi ya mchanganyiko wa tende maalum yaani maziwa, asali na unga wa hiriki huweza kuwa msaada kwa wale wenye shida ya nguvu za kiume. Kule Zanzibar unaweza kuipata kama juice kwenye maeneo mengi ikiwa na mchanganyiko huu
Tende vile vile huimarisha nuru ya macho na tatizo la kutokuona usiku (night blindness).
Kutokana na wingi wa virutubisho vilivyomo, tende huweza pia kutibu magonjwa mengine ya tumbo, yakiwemo kujaa gesi, kuharisha na kuchafuka kwa tumbo. Kwa wale walevi wa kupindukia, ambao miili yao imejaa sumu, tende huweza kuwa na msaada mkubwa wa kuondoa sumu hizo katika miili yao.
Nachoweza kusema ni kwamba kuna faida nyingi za tende na unaweza kuila tende kwa namna mbalimbali, kama vile kuchanganya na maziwa, kuchanganya na mkate au vitafunwa vingine. Ifanye tende kuwa sehemu ya mlo wako wa kila siku ili ujipatie faida hizi 10 na nyingine. Hivyo basi, tende isiliwe mwezi wa Ramadhani peke yake, bali iwe ni chakula ama tunda la kuliwa wakati wote na watu wote, kwa sababu kila mtu anahitaji kuwa na afya bora
Bado Tende Linabaki kuwa tunda asilia kabisa kwa kuwa halijaghoshiwa bado (GMOs)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...