Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya kupokea madawati yaliyoyolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma shule bunge mwaka 1991 leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Shule ya msingi Bunge, Khadija Telela akisoma hotuba kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa hafla ya kupokea madawati yaliyoyolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma shule bunge mwaka 1991 leo jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule ya bunge wakiwa katika furaha baada ya kupokea madawati katika hafla ya kupokea madawati yaliyoyolewa na Umoja wa Wanafunzi waliosoma shule bunge mwaka 1991 leo jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
UMOJA wa wanafunzi waliohitimu shule ya msingi bunge mwaka 1991 wameikomboa shule hiyo kwa kutoa msaada wa madawati 70 yenye thamani ya milioni saba.
Akizungumza na wakati wa makabidhiano ya madati hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kuwa wanafunzi waliosoma bunge wametambua umuhimu wao katika kusaidia shule waliosoma kwa kwenda na kampeni ya madawati katika Mkoa wa Dar es Salaam.
Makonda amesema kila mmoja kwa makundi waliosoma shule zao wanawajibu wa kwenda kusaidia katika mapungufu katika shule hizo.
Aidha amewataka wanafunzi kuiga mfano wa wanafunzi wenzao waliosoma hapo kuwa wakihitimu wanaweza kutatua baadhi ya changamoto katika shule ya bunge.
Mwenyekiti wa umoja wanafunzi waliohitimu mwaka 1991, Eliapenda Lyimo amesema kuwa wametambua kampeni ya madawati katika mkoa wa Dar es Salaam kuona shule ya bunge wanauhitaji wa madawati.
Eliapenda amesema kuwa shule ya bunge kwa msaada wa madawati hayo bado wanaupungufu wa madawati 50 ambapo wakipata madawati hayo, shule itakuwa imeachana upungufu wa madawati.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...