Ziara ya Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania (Tanzania
Saccos for Women Enterprenuers) imezaa matunda baada ya kikundi hicho kufanikiwa kuingia mkataba wa ushirikiano (MoU) katika masuala
ya biashara na Kikundi cha Wanawake Wajasiriamali wa Comoro (Association
of Women Entreprenuers in Comoro).
Makubaliano hayo ya ushirikiano yalifikiwa kufuatia ziara ya siku mbili iliyofanywa
na Kikundi cha Wajasiriamali Wanawake kutoka Tanzania nchini Comoro tarehe
14 Juni 2016. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kutafuta masoko kwa ajili ya bidhaa za
Tanzania nchini Komoro, pamoja na kukutana na wajasiriamali wa Komoro ili
kuweza kubadilishana taarifa juu ya fursa mbalimbali za biashara kati ya
Tanzania na Comoro.
Tukio hilo la utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano baina ya vikundi hivyo vya
Wajasiriamali akina mama kutoka Tanzania na Comoro lilishuhudiwa na Balozi
wa Tanzania nchini Komoro Mhe. Chabaka F. Kilumanga. Katika hafla hiyo,
Mhe. Balozi Kilumanga aliwapongeza wajasiriamali hao kwa hatua hiyo
muhimu waliofikia na kuwa ana imani ushirikiano huo utakuwa ni wakudumu na
wenye manufaa kwa pande zote mbili.
Alieleza kuwa Tanzania na Comoro
zinaweza kushirikiana katika nyanja mbalimbali za biashara na ana imani kuwa
hii itakuwa ni chachu kwa wawekezaji wengine kutoka Tanzania kuja nchini Comoro kwa ajili ya kuekeza.
Balozi wa Tanzania nchini Comoro, Chabaka F. Kilumanga na Bw. Mudrick Soragha Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania Komoro wakishuhudia utiaji saini mkataba wa ushirikiano baina ya vikundi vya wajasiriamali wanawake kutoka Tanzania na Komoro.
Bi. Naila Thabeet wa Association of Women Enterpreneurs akibadilishana mkataba na Bi. Anna Matinde kutoka Tanzania Saccoss for Women Enterprenuers.
Wadua wakishuhudia tukio la kihistoria ambapo ni mara ya kwanza vikundi vya akina mama kutoka Komoro na Tanzania wamekubaliana kushirikiana katika nyanja za biashara.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...