Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akiongea na wazee katika kituo cha Nkaseka Mkoani Mtwara na kumshukuru Mtumishi wa Mungu TB Joshua kuunga mkono juhudi zake za kuwasaidia wazee na watu wasiojiweza kwa kuchangia baadhi ya vitu vilivyotolewa kama msaada kwenye kituo hicho.
 Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa akiongea na Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
 Muwakilishi wa Mtumishi wa Mungu TB Joshua Nchini Tanzania Mhandisi Consolata Ngimbwa akitoa salamu kutoka kwa TB Joshua aliyetoa msaada kwa ajili ya wazee wa kituo cha Nkaseka kilichopo Wilayani Masasi Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akimkabidhi Kiongozi wa Wazee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka Bw. Boniface Mbedo misaada leo Mkoani Mtwara.
 Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na moja ya Mzee wa Kituo cha Kulea Wazee cha Nkaseka baada ya kumpa zawadi ya Ungo, Chungu na Mwiko. Kulia ni Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa, wakati wa hafla ya utoaji misaada kwenye kituo cha kulea wazee na watu wasiojiweza cha Nkaseka Mkoani Mtwara.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...