BARA la Afrika limetakiwa kuimarisha Utawala wa Sheria kupitia vyombo vya
dola ikiwemo mahakama na polisi ili kuisaidia mfumo huo kutetea maslahi ya
wanyonge.
Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Augustine Mahiga wakati alipokuwa
akifunga Mkutano wa siku mbili wa Kimataifa kuhusu Utawala wa Sheria na
Utawala bora.
“Lazima Afrika iimarishe vyombo vyake vinavyosimamia Utawala wa sheria na
Utawala bora kama Polisi na Mahakama pamoja na kuwa na msimamo wa Bara
katika kuzungumzia masuala mbalimbali” alisema Balozi Mahiga
Balozi Maiga alisisitiza kuwa rushwa imekua adui mkubwa katika Utawala wa
Sheria, hivyo ni lazima suala hilo lipatiwe ufumbuzi ili haki iweze kutendeka kwa
watu wote.
Aidha, Balozi Maiga amemshukuru Balozi wa Italia nchini Mhe. Luigi Scott kwa
kufanikisha mkutano huo pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la
Maendeleo ya Sheria (IDLO) Bibi. Irene Khani kwa uamuzi wa wake wa
kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo.
“Mkutano huu ni wa kihistoria utasaidia kuleta mageuzi katika Taasisi ama
Vyombo vinavyosimamia masuala ya Sera na Sheria ambayo yatachochea
maendeleo mazuri katika nchi za Afrika” alisema Balozi Mahiga.
Mkutano huo unaomalizika leo ulikua na kauli mbiu isemayo “Kufikia agenda ya
2030 na agenda ya 2063: Utawala wa Sheria kwa Maendeleo Endelevu ya Afrika”,
umehusisha wadau mbalimbali wakiwemo Mawaziri, kutoka nchi mbalimbali za
Afrika, Mabalozi kutoka ndani na nje ya Afrika pamoja na wawakilishi wa
Mashirika ya kutetea Haki za Binadamu ulimwenguni.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki Balozi Augustine
Maiga akitoa maelezo kwa wadau waliohudhuria mkutano wa Utawala wa Sheria
na Utawala Bora (hawapo pichani) uliofanyika leo jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine
Maiga akiongea jambo na Balozi wa Italia Nchini Mhe. Luigi Scotto baada ya
kumaliza mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora uliofanyika leo jijini
Dar es salaam.
Wadau wa Mkutano wa Utawala wa Sheria kutoka nchi mbalimbali duniani
wakifatilia kwa makini mkutano wa Utawala wa Sheria na Utawala Bora ili
kufikia agenda ya mwaka 2030 na 2063 ya malengo ya millennia uliofanyika leo
jijini Dar es salaam.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...