Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe)
akizindua Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane
kuyatumbua leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia ni Mjumbe wa Kamati ya
Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Bi. Deborah Charles, Agusto Matefu,
Mwenyekiti wa Kamati ya Mijadala na Kongamano ambaye pia ni Mwandishi wa
kitabu hicho Amos Siyantemi na wa mwisho kushoto ni Mratibu wa Taifa wa
Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda. Kampeni
hiyo inalengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika
jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.
Makamu
Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula(mwenye shati jeupe) akionyesha
Kitabu chenye jina la “Majipu ya Nchi Yetu” Tushirikiane kuyatumbua mara
baada ya kukizindua leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) ambaye pia
ni Mwandishi wa kitabu hicho Amos Siyantemi na kushoto ni Mratibu wa
Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini (KVM) Bw. Daniel Zenda.
Kampeni hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli
katika jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa
majipu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM) Amosi Siyantemi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa uzinduzi
wa Kitabu cha Majipu ya Nchi yetu “ Tushirikiane kuyatumbua leo jijini
Dar es Salaam. Katikati ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula
na kushoto Mratibu wa Taifa wa Kampeni ya Vitabu na Midahalo nchini
(KVM) Bw. Daniel Zenda.
Waandishi wa habari wakifuatilia uzinduzi wa Kitabu cha Majipu ya Nchi
Yetu “Tushirikiane kuyatumbua” leo jijini jijini Dar es Salaam. Kitabu
hiko kimezinduliwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara Philip Mangula
(hayupo pichani).Uzinduzi wa Kitabu hicho umeenda sambamba na
utambulisho wa Kamati ya Kampeni ya Vitabu na Midahalo (KVM). Kampeni
hiyo ina lengo la kumuunga mkono na kumsaidia Rais Magufuli katika
jitihada zake za kupambana na rushwa maarufu kama utumbuaji wa majipu.Picha zote na: Frank Shija, MAELEZO.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...