Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa juu ya haki za watu wenye ualbino, Ikpowose Ero, akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam jana juu ya maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa watu wenye ualbino Afrika uliofanyika nchini hivi karibuni, Kushoto ni Mwakilishi Mkazi wa UN, Alvaro Rodrigers na Mkurugenzi mkazi wa Under the same  Sun.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
SERIKALI imeaswa kupiga vita dhidi ya  ukatili, unyanyapaa pamoja na  mauaji Watu Wenye Ualbino ili kuweza  kila mtu kuishi kwa amani katika nchi yake.  

Katika kupiga vita dhidi ukatili na unyanyapaa ya watu wenye Ualbino ni kuweka mkakati wa kuandaa mashitaka kwa ubora zaidi dhidi ya uhalifu wa Ualbino ,kuandaa kanuni za kusimamia waganga wa jadi pamoja na kuimarisha kampeni maalum na endelevu za ufahamu kwa miaka miwili mfululizo ili kupunguza vifo vitavyotokea mara kwa mara.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar  es Salaam uliohusisha  nchi  29  Kanda ya Afrika,Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa, Ikponwosa Ero, amesema mauaji ya watu wenye Ualbino  yanaendelea kutokea Barani Afrika na kufanya jamii hiyo kukosa haki ya kuishi  kutokana mauaji dhidi yao.
  
Amesema  kuna matukio mengi dhidi ya watu wenye ualbino  lakini yamekuwa hayaripotiwi kwa sababu ya usiri katika masuala ya ushirikiana,ushiriki wa familia na ushiriki wa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha.

Naye, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga amesema serikali inatakiwa kuongeza bajeti yake ili watu wenye Ualbino wapate haki sawa katika masuala ya matibabu.

 “Serikali ihakikishe kuwa vifaa vya kuimarisha uwezo wa kuona vinapatikana kwa ajili ya mtu m wenye ualbino  anapokuwa darasani na kutoa vizuia jua nafuu kama tiba muhimu ili kuziua saratani ya ngozi, ambayo inaendelea kuondoa maisha ya watu hao”amesema Nyanduga.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa The Under Sun (TUS), Vick Mtetema amesema kwa pamoja wataendelea kupambana na unyanyapaa na mauaji dhidi ya watu wenye ualbino.

Amesema polisi wa kimataifa na watu wa Uhamiaji washirikiane kwa pamoja ili kulinda watu wanaopitisha watu wenye Ualbino.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 20, 2016


    Hili swala la mauaji ya watu wenye ualbino ni kweli linahitaji msukumo mkubwa na ushirikiano mpana. Hata hivyo naamini ni ishara ya kushindwa kwa utawala bora pale ambapo taasisi za nje tu ndio zinaonekana kuliwekea kipaumbele. Taasisi zetu kama Chama cha Watu wenye Ualbino Tanzania ziko wapi. Mbona wamegawanyika na kuwaachia wageni tu sauti zao kusikika. Hao Under the Same Sun wametoka nchi gani? Tuimarishe Vyama vyetu ili tuwe na ubia mkubwa katika vita hivi. Nashangaa hata Waziri mwenye wajibu wa hili ambaye ni mtu mwenye ualbino halioni. Tusipokuwa na kauli moja na Taasisi imara za kwetu wageni watakuwa wanatumia watu wetu na vyombo vyetu kujitafutia umaarufu tu wakati tatizo linabakia palepale.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...