Na Mbaraka Kambona,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju amesema kuwa mapenzi ya jinsia moja hayakubaliki na Serikali ilishaweka msimamo wake katika hilo.
Akizungumza mapema  katika mkutano wa wadau wa haki za binadamu uliofanyika katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es salaam  kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu (Universal Periodic Review) na kuweka mikakati ya kuishawishi serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa, Mhe. Mpanju ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo alisema  mapendekezo yaliyowasilishwa Mwezi Mei mwaka huu katika mkutano wa Baraza la haki za binadamu uliofanyika Geneva, serikali ilikubali mapendekezo Mia thelathini (130) na mengine 72 iliyakataa.
“Sehemu ya mapendekezo hayo serikali iliyakataa kwa sababu kuna mengine yapo kinyume na katiba, sheria, mila na desturi zetu, kwani katika mapendekezo hayo yapo yanayotaka mapenzi ya jinsia moja jambo ambalo haliwezi kukubalika”, Mhe. Mpanju alisema
“Hivyo wakati mkijadili namna ya kupanga mikakati ya utekelezaji ili serikali ione umuhimu wa kukubali sehemu ya mapendekezo hayo naomba msijielekeze kwenye yale yaliyo kinyume na imani”, Mhe. Mpanju alisisitiza 
Aidha, Mhe. Naibu Katibu huyo alisema serikali imefungua milango kwa kushirikiano na tume, wadau wa haki za binadamu wapeleke serikalini  sababu zenye mantiki ili kuona ni mambo gani  ambayo serikali inaweza  kuyashugulikia na kuyatekeleza.
Akizungumza katika Mkutano huo, Bwana Onesmo Olengurumwa kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) alisema kuwa wadau wamekutana katika mkutano huo   kujadili ni kwa namna gani wataishawishi serikali ili iweze kuyakubali mapendekezo yaliyobakia na kuyaweka katika utekelezaji.
Akitoa muhtasari wa  mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Iddi Mapuri alisema kuwa mkutano huo umelenga katika kuweka mikakati ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa mapendekezo hayo na alipongeza mchango mkubwa unaotolewa na wadau wa haki za binadamu katika kuhakikisha masuala ya haki za binadamu yanapata msukumo mkubwa hapa nchini.
 Bwana Onesmo Olengurumwa (kulia) kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) akijadiliana jambo na Mkurugenzi  wa Idara ya huduma za sheria wa Tume ya Haki za Binadamu, Bwana Nabor Assey( aliyevaa shati la bluu). Nyuma yao ni Bwana Laurent Burilo Burilo, Mratibu wa Mpango kazi wa Haki za Binadamu(katikati) na Bwana Deugratius Bwire kutoka (THRDC.
 
 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Mhe. Iddi Mapuri akisoma muhtasari wa mkutano huo kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju (kulia) akiteta jambo na Bwana Onesmo Olengurumwa kutoka taasisi ya watetezi wa haki za binadamu (THRDC) katika mkutano huo wa  kujadili mapendekezo ya tathmini ya utekelezaji wa masuala ya haki za binadamu na kuweka mikakati ya kuishawishi serikali kukubali mapendekezo mengine ambayo iliyakataa.
Wadau walioshiriki mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Mhe. Amon Mpanju.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...