Marekani yasawazisha makosa yake ya mchezo wa kwanza wa mashindano ya Copa America ilipofungwa mabao 2-0 na Colombia, kwa kisambaratiaha Costa Rica kwa mabao 4-0, katika mchezo uliopigwa jijini Chicago. Hadi mapumziko Marekani walikuwa mbele kwa mabao 3-0 yaliofungwa na Clint Dempsey kwa mkwaju wa penati, hili lilikuwa goli lake la 10 kwa timu yake ya taifa. Goli la pili lilifungwa na Jermaine Jones dakika ya 37 na dakika 5 baadaye Bobby Woods akafunga goli la 3.

Karamu ya magoli ilihitimishwa na Graham Zusi aliyeingia kuchukuwa nafasi ya Bobby Woods, kwa kufunga bao la 4 katika dakika ya 87 ya mchezo.
Wakati huo huo Colombia imejihakikishia nafasi ya kusonga mbele hatua ya mtoano baada ya kuifunga Paraguay mabao 2-1. Colombia sasa wamejikusanyia pointi 6 kwa kushinda michezo yake miwili. Iliwachukuwa dakika 10 kujipatiabao la kuongoza lililofungwa na Carlos Bacca akiunganisha kwa kichwa mpira wa kona iliyopigwa na James Rodriguez. Dakika ya 29 James Rodriguez aliipatia timu yake bao la pili.

Paraguay walijipatia bao la kufutia machozi kunako dakika ya 70 lililowekwa kambani na Ayala Golazo kwa shuti kali la umbali wa mita 25,goli hili limeonekana kuwa ni goli bora kwa mechi zote ambazo zimekwisha chezwa.

Leo kutakuwa na michezo ya kundi B

BRAZIL vs HAITI
EQUADOR vs PERU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...